Mwakilishi wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) anayefanyia kazi nchini Tanzania Andrew Rebold, akielezea kufurahishwa kwake na juhudi zinazochukuliwa juu ya kutokomeza Malaria Zanzibar (kulia) Naibu Waziri wa Afya Dk. Sira Ubwa Mamboya, Afisa wa RTI kanda ya Afrika Mashariki Volkan Cakir kabla yakukabidhi pikipiki 10, huko katika uwanja wa Wizara ya Afya nje Mjini Zanzibar.
Baadhi ya maafisa mbalimbali wa Wizara ya Afya wakimskiliza Mwakilishi wa Shirika la Misaada laMarekani (USAID) anayefanyia kazi nchini Tanzania Andrew Rebold (hayupo pichani) katika uwanja wa Wizara ya Afya nje Mjini Zanzibar.
Mwakilishi wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) anayefanyia kazi nchini Tanzania Andrew Rebold akimkabizi helmet na pikipiki Naibu Waziri wa Afya Dk. Sira Ubwa Mamboya kwa ajili ya Afisa Wilaya wafuatiliaji wagonjwa wa Malaria, katika uwanja wa Wizara ya Afya nje Mjini Zanzibar.
Naibu Waziri wa Afya Dk. Sira Ubwa Mamboya akimkabizi funguo ya pikipiki mmoja wa Afisa Wilaya wa ufuatiliaji wagonjwa wa Malaria, huko katika uwanja wa Wizara ya Afya nje Mjini Zanziba

(Picha zote na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar)
Na Salum Vuai, Maelezo
MFUKO wa Rais wa Marekani unaoshughulikia mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria katika nchi mbalimbali za Afrika (PMI), umekabidhi pikipiki kumi kwa Wizara ya Afya Zanzibar, zitakazotumika kufuatilia kesi za malaria katika wilaya zote Unguja na Pemba.
Hafla ya makabidhiano ya pikipiki hizo zenye thamani ya shilingi milioni 63 amabzo ni maalumu kwa ajili ya Kitengo cha Kupambana na Malaria Zanzibar, ilifanyika jana huko Wizara ya Afya Mnazimmoja na kuhudhuriwa na watendaji mbalimbali wa wizara hiyo.
Mwakilishi wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) anayefanyia kazi nchini Tanzania Andrew Rebold, alisema pikipiki hizo zitasaidia kazi za kufuatilia kesi za malaria majumbani, ambako familia zitapimwa ugonjwa huo na kupatiwa tiba inapobidi.
“Hii ina maana kuwa, maofisa wenu wa malaria mawilayani, wataongeza uwezo wao katika kufuatilia, kuchunguza, kutibu pamoja na kukinga ugonjwa huo kwa kuhakikisha kwamba wananchi wanaogundulika nao wanatibiwa haraka iwezekanavyo, na kusaidia kuvifanya visiwa vya Zanzibar kutokuwa na malaria”, alisema.
Rebold alieleza kuwa, tangu PMI ilipoanzishwa mwaka 2006, pamoja na washirika wake wengine ikiwemo RTI, wmaefanya kazi kwa karibu na Wizara ya Afya Zanzibar na Tanzania Bara kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa malaria.
Alifahamisha kuwa, misaada ya kitaalamu na ya kifefha kutoka mfuko huo wa Rais wa Marekani, imeisaidia Zanzibar kupunguza ugonjwa wa malaria kutoka asilimia 25 mwaka 2006 hadi kufikia chini ya asilimia moja mwaka 2009, na kwamba mafanikio hayo yamekuwa endelevu.
“Mafanikio haya ni kielelezo cha uhusiano na ushirikiano madhubuti kati ya PMI na Serikali ya Zanzibar, sambamba na uongozi imara wa serikali yenu”, alieleza Rebold.
Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Afya Dk. Sira Ubwa Mamboya, alisema kwa kuwa kazi ya kupambana na malaria inahitaji ufuatiliaji wa mara kwa mara, pikipiki hizo zitawarahisishia maofisa wa kitengo cha malaria mawilayani kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na wepesi.
Alisema msaada huo ni faraja kwani utatia fursa kwa watu wanaogua malaria hasa walioko vijijini, kupatiwa tiba kwa wakati pamoja na watu wanaoishi nao kuchunguzwa ili kubaini kama wameathirika na kuwezesha kutibiwa kwa wakati.
Kwa niaba ya serikali, Dk. Sira alishukuru kwa msaada huo na mingine inayotolewa na PMI, RTI na USAID, ambayo alisema imeifanya Zanzibar kupunguza malaria kwa kiasi kuwa na kuwa mfano kwa nchi nyengine.
Mapema Afisa wa RTI kanda ya Afrika Mashariki Volkan Cakir, aliipongeza Zanzibar kwa hatua kubwa iliyopiga na kupunguza malaria kwa kiwango cha chini ya asilimia moja, na kusema taasisi yao inaona fahari kuwa sehemu ya mafanikio hayo.
0 comments:
Post a Comment