Thursday, August 15, 2013


Makamu-wa-Rais-Mazingira-Dk-Terezya-HuvisaNa Gervas Charles Mwatebela, Dar es salaam
Serikali imepiga marufuku uingizaji, utengenezaji, uuzaji, na utumiaji  wa mifuko ya plastiki. hayo yameelezwa  na Waziri  wa nchi ofisi  ya makamu wa Rais(mazingira) Dk Terezya Huvisa  alipokuwa akizungumza na waandishi ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
 Dkt. Huvisa ameeleza kuwa Serikali imehamua  kuchukua hatua hii ili kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo la kusambaa na kutapakaa kwa taka za mifuko ya plastiki ambayo baada ya matumizi yake huishia kwenye uchafuzi  wa mazingira .
Amesisitiza kuwa, Zuio hili linahusu mifuko yote ya Plastiki ya kubebea bidhaa toka madukani, sokoni na majumbani isipokuwa mifuko yenye unene wa maikroni mia moja inayooza (bio-digradable) na  vifungashio vya bidhaa mbali mbali kama vile vifaa vya mahospitalini.
Dkt Hufisa aliendela kusema kuwa, Jitihada zinatakiwa zifanywe ili kuhakikisha kuwa marufuku hii inazingatiwa, na misako ya watu wanaofanya biashara ya mifuko hii ifanyike katika maeneo yote ndani ya nchi yetu, na watakaokiuka wachukuliwe hatua, ikiwa ni pamoja na kufanikishwa katika vyombo vya sheria .
Imeelezwa kuwa madhara yanayosababishwa na mifuko ya plastiki ni pamoja na uharibifu wa udongo unaotokana na kuunguzwa kwa plastiki hizi na hivyo kusababisha madhara ya kiafya kwa binadamu na wanyama ,kutooza kiurahisi wa njia za kiasili (non-biodegradable) kuzagaa katika mito, maziwa, bahari na nchi kavu hivyo kuhatarisha maisha ya viumbe hai wanaoishi katika mazingira.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video