Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
KLABU ya Tottenham imetangaza kukamilisha usajili wa kiungo mahiri kutoka klabu ya Ajax, Christian Eriksen kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 11.5.
Usajili huo wa Spurs dakika hizi za majeruhi wenye nia ya kufanya makubwa msimu huu ni watatu na wasaba kwa majira haya ya kiangazi
Nyota huyo wa kimataifa Raia wa Denmark amejiunga na beki wa Kiromania, Vlad Chiriches aliyesajiliwa kwa dau la £8.5m na mshambuliaji Raia wa Argentina, Erik Lamela aliyesajiliwa kwa dau la £30m na usajili wake kwa wakali hao wa kaskazini mwa London umekamilika jana Ijumaa.
“Tunafurahi kutangaza kuwa tumefikia makubaliano na Ajax juu ya uhamisho wa Christian Eriksen,’”, Spurs wamesema katika mtandao wao wa kiofisi ” official website.”
Kiungo mahiri: Eriksen alionekana katika mazoezi ya Spurs hapo jana
Watatu hao wanajiunga na wenzao wapya Paulinho (£17m), Nacer Chadli (£6m), Roberto Soldado (£26m) na Etienne Capoue (£8.6m) ambao wamewasili dimba la White Hart Lane majira haya ya kiangazo.
Eriksen alisema: Kila mtu anafuatilia maendeleo ya Spurs, kitu ambacho hata mimi nataka kuwa sehemu yake.’
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21, tayari ameshaichezea timu yake ya taifa mara 37 na kufunga mabao 4 na alikuwa mchezaji muhimu wa Ajax ambako alijiunga mwaka 2008 akitokea klabu ya Odense .
Ijumaa njema zaidi: Chiriches alionekana jana wakuwa Spurs
0 comments:
Post a Comment