Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
KILA mtu anakumbuka mwezi Disemba mwaka jana ambapo mchezaji wa Swansea City, Ashley Williams alimfanyia rafu mbaya mashambuliaji wa Manchester United Robin Van Persie baada ya kucheza mpira kichwani kwa Mholanzi huyo.
Kocha Sir Alexxz Fergusons alimshutumu kuwa alitaka kumuua ARV, Sasa leo hii wawili hao wanakutana tena muda mfupi ujao katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu England ambapo Swansea wanawakaribisha United katika dimba lao la Liberty Stadium.
Katika mchezo huo wa mwaka jana timu hizo zilitoka sare ya 1-1 na Ferguson aligeuka mbogo kutokana na nyota wake kufanyiwa kitu mbaya, lakini Williams alikiri na kusema ilikuwa ajali tu ya uwanjani na hakukusudia.

Lakini Williams amesisitiza kuwa katika mchezo wa leo ataangalia zaidi kazi yake na watakapokutana na Robin Van Persie hatatishika na nyota huyo wa United.
Williams amesema: ‘Robin ni mchezaji mkubwa na ndio maana natakiwa kumkaba vizuri – siku zote napenda kucheza na wachezaji wa bora zaidi na kujaribu kuwanyamazisha.’

Ajali: Williams amesisitiza kuwa hakukusudia kumchezea vibaya Van Persie

Mtu hatari: Van Persie alifunga mabao yote mawili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Wigan na kutwaa kombe la ngao ya Hisani
0 comments:
Post a Comment