Saturday, August 10, 2013


IMG_0247Betram Mombeki ni hatari sana, leo hii ametupia mawili katika ushindi wa mabao 4-1
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Hatimaye Tamasha la “Simba Day” lanoga uwanja wa Taifa ambapo Wekundu wa Msimbazi Simba leo hii wamecheza mechi ya kirafiki dhidi ya miamba ya soka la Uganda, Sports Club Villa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam ikiwa ni mechi maalumu ya siku ya Simba “Simba Day” inayofanyika  Agosti 8 kila mwaka, lakini mwaka huu wamelazimika kuifanya Agosti 10 kutokana na kuingiliana na sikukuu ya Idd El Fitri.
Mechin hiyo kali iliyopigwa mbele ya wanachama, mashabiki na viongozi wa Simba na wa timu pinzani ilikuwa kali ya kusisimua huku Kikosi cha Simba kikicheza soka safi, lakini mpaka dakika dakika 45 zikimalika, miamba hiyo ya soka la Afrika mashariki na kati ilikuwa imechoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1, huku waganda wakiwa wa kwanza kufunga bao lao.
Simba walisawazisha mufa mfupi kabla ya kwenda mapumziko kupitia kwa nyota wake kinda Gerrard Jonas Mkude na kuibua shangwe na nderemo kubwa kwa mashabiki wa Simba.
 Kipindi cha pili Simba walianza kwa kasi na kuonesha soka safi la kufundishika huku mashabiki wake wakishangilia kwa nguvu zote kutokana  utaalamu mwingi wa kikosi chao kinachonolewa na kocha mzalendo, Abdallah King Kibaden Mputa.
Wekundu wa Msimbazi waliongeza bao la pili katika dakika ya 9 kipindi cha pili, kupitia kwa kinda lao, Wiliam Lucian aliyepiga shuti kali na kutinga nyavuni.
Katika dakika ya 25 kipindi cha pili, Betram Mombeki aliandika bao la tatu na kuzidi kuwapa raha mashabiki wa Simba waliokuwa wanashangilia kwa staili ya kuwakejeli mashabiki wa upande wa pili walioonekana kuwa kimya muda mwingi.
Katika dakika ya 28, Mombeki aliandika bao la nne na kuonekana kama dawa halisi ya kufunga mabao kwa wekundu wa Msimbazi Simba kwa lugha ya mtaani “Mtambo wa magoli”.
Leo hii bila kupepesa macho, Mnyama ameonesha kiwango kikubwa zaidi ukilinganisha na mechi za kirafiki walizocheza huko nyuma.
Beki wa kati waliyemsajili kutoka URA ya Uganda alionekana kuimarisha safu ya ulinzi ya Simba ingawa alitolewa dakika za mwisho kipindi cha pili, lakini Mombeki ambaye alitolewa pia na nafasi yake kuchukuliwa na Ramdhan Singano “Messi” alikuwa moto wa kuotea mbali kwa kutupia kambani mabao mawili.
Kila Simba wanapokutana na majogoo wa Kampala, Sports Club Villa iwe ni mechi ya kirafiki au mashindano, huwa upinzani unakuwa mkubwa sana kwani zina historia kubwa na ushindani wa muda mrefu.
Lakini leo,  Simba wamewazidi sana wanaume hao wa Uganda na kuwaburuza bao 4-1 na hivyo Simba wamerejesha furaha kwa mashabiki wao ambao kwa muda mrefu hawajashuhudia timu yao ikifanya vizuri.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video