Na Baraka Mpenja
Wakati harakati za kujiandaa na ligi kuu soka Tanzania bara zikiendelea kwa klabu mbalimbali, Wekundu wa Msimbazi Simba kesho wanatarajia kucheza mechi ya kirafiki uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam dhidi ya Kombaini ya maafande wa Polisi.
Akizungumza na MATUKIO DUNIANI , Afisa habari wa Simba, “Mr. Liverpool”, Ezekiel Kamwaga, amesema maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika na wachezaji wote wa klabu hiyo, wa zamani na wapya wote wapo salama, hivyo ni nafasi kwa wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kwenda kuona soka la wanandinga wapya.
“Mechi itakuwa nzuri sana, timu zote zimejiandaa vizuri, hivyo kwa wale watakaofika uwanjani kwa watafurahia kwa maana ya matokeo au soka maridadi”. Alisema Kamwaga.
Kamwaga aliongeza kuwa mchezo wa kesho utawatambulisha baadhi ya wachezaji wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao, lakini Amis Tambwe hatakuwepo kwani hajawasili nchini Mpaka sasa.
“Kuhusu Tambwe, kiukweli hatakuwepo, lakini tunatarajia kuwa naye siku ya “Simba Day” kuonesha makali yake aliyotoka nayo katika kombe la Kagame”. Alisema Kamwaga.
Simba itashuka dimba la taifa kwa mara ya pili tangu kumalizika kwa ligi kuu soka Tanzania bara mei 18 mwaka huu, ambapo mechi ya kwanza walicheza na URA ya Uganda na kufungwa mabao 2-1, hivyo mechi hiyo ni muhimu sana kwao kuwafurahisha wapenzi wao.
0 comments:
Post a Comment