Tuesday, August 20, 2013

IMG_1696Naibu Waziri Bilinith Mahenge akiwa anangalia kisimacha maji
kinachochimbwa Wilayani Karatu mkoani Arusha wiki iliyopita (Picha na
Gladness Mushi, Arusha)
………………………………………………………..
Na  Gladness Mushi wa Fullshangwe-Arusha
SERIKALI imesema kuwa itaboresha miundombinu ya Visima vya maji hasa
katika maeneo ambayo yana visima lakini vinashindwa kutumika kutokana
na ubovu pamoja na uchakavu wa miundombinu ya visima hivyo
Aidha miundombinu ikishaboreshwa itasaidia kwa kiwango kikubwa sana
kuweza kupunguza tatizo la uhaba wa maji hasa maeneo ya   vijijini na
hivyo kuweza kuongeza uzalishaji katika sekta zote ndani ya jamii
Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri wa Maji DktBillinith Mahenge
wakati akiongea na wadau wa maji katika Halmashauri ya Monduli mapema
jana (leo)ambapo alidia kuwa mpango huo kwa sasa upo kwenye maandalizi
ya hatua za mwisho na utaanza hivi karibuni
Dkt Billinith alisema kuwa,katika Nchi ya Tanzania kuna visima vingi
sana ambavyo kama vingeweza kutumika ipasavyo basi vingechangia tatizo
la uhaba wa maji kupungua lakini mpaka sasa baadhi ya visima
vinashindwa kutumika kutokana na ubovu wa miundombinu
Alifafanua kuwa serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha
kuwa miundombinu yote ya visima vya maji itaboreshwa na visima vyote
vilivyojengwa kwa makusudio ya kuwasaidia wananchi viweze kutumika ili
kufikisha malengo ndani ya jamii
“tunataka kila kisima kilichowekwa kwa makusudio ya kuwasaidia
wananchi kiweze kutumika na kusiwe na utaratibu wa kuchimba kisima
kama mazoea uweze kuisha kwani unafanya malengo yua kupambana na uhaba
wa maji uweze kuisha kabisa hapa nchini”aliongeza dkt Billinith
Katika hatua nyingine aliitaka halmashauri ijiwekee utaratibu wa
kutafuta na kubuni vyanzo vya mapato hasa kwenye sekta ya maji ili
kuweza kuraisisha shuguli za maji kwani bado Wilaya hiyo inakabiliwa
na matatizo ya uhaba wa maji
Katika hatua nyingine mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya
Monduli,Twalibu Mbasha alidai kuwa pamoja na kuwa wamejitaidi huduma
za maji kuwafikia wananchi wengi wa wilaya hiyo lakini bado kityengo
cha maji hakina wataalamu  wa  kutosha
Mbasha alisema kuwa idadi ya wataalamu waliopo kwenye sekta ya maji
ni wachache  sana huku pia baadhi ya huduma za Halmashauri kukwama
hivyo basi Serikali inatakiwa kuongeza idadi ya wataalamu ili huduma
hiyo ya Maji iweze kuwafikia wananchi wote.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video