Friday, August 9, 2013


Na Baraka Mpenja 
Maafande wa Ruvu Shooting  chini ya kocha Charles Boniface Mkwasa “Masta” wanazidi kuwavutia kasi Tanzania Prisons “Wajelajela”  katika mchezo wao wa ufunguzi wa ligi kuu soka Tanzania bara utakaopigwa uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani agosti 24 mwaka huu.
Akizungumza na mtandao wa MATUKIO DUNIANI,  Afisa habari wa klabu hiyo, Masau Bwire amesema maandalizi yanakwenda vizuri, wachezaji wote wanaisubiri kwa hamu mechi ya ufunguzi kwani wana uhakika kuibuka na ushindi kutokana na maelekezo mazuri ya kocha Mkwasa.
“Vijana wetu wanaimarika kila kukicha, malengo yetu ni kushika nafasi tatu za juu katika msimamo wa ligi kuu, tumechoka kuwaachia Simba na Yanga kama mbio za kupokezana vijiti, hakika tunajiwinda vikali sana”. Alisema Masau.
RUVU SHOOTINGKikosi cha Ruvu Shooting msimu uliopita
Masau alisema kwa sasa kocha wao anafanya jitihada kubwa kunoa safu ya ushambuliaji ambayo msimu uliopita ilikuwa tatizo kwao, ingawa kwa upande Mkwasa alikaririwa na mtandao huu kuwa bado tatizo la ushambuliaji ni la taifa zima kwani timu zote zinakabiliwa na safu butu ya ushambuliaji.
Afisa habari huyo alisisitiza kuwa mpira wa miguu ni wa makosa, lakini wanajitahidi kufuta makosa yanayoweza kuwazuia kutimiza ndoto zao msimu ujao,  hivyo lazima mashabiki wawe na imani kubwa na kikosi chao.
“Sisi tunataka kuwa watu wa kwanza kutibua ufalme wa Simba, Yanga, hata wao wanajua jinsi shughuli yetu ilivyo, tunapiga mpira mzuri sana, ikumbukwe msimu uliopita sisi tulikuwa timu ya kuotea mbali kwa kucheza soka zuri na wadau waliona, lakini waamuzi walituangusha sana”. Alisema  Masau.
simba5Unaikumbuka shughuli hii ya Ruvu Shooting dhidi ya Simba msimu uliopita? sasa wamesema wataongeza zaidi
Masau aliwataka mashabiki wa soka wa mkoa wa Pwani kuondoa shaka kwa sasa kwani kikosi kinasukwa vizuri sana, na kocha wao mtaalamu Mkwasa anawafua wachezaji kwa kuwapatia mbinu mpya na ikizingatiwa wameongeza nguvu kwa kusajili wachezaji wakali akiwemo Stephano Mwasyika kutoka Yanga na Elias Maguli kutoka Tanzania Prisons ya Mbeya.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video