Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mshambuliaji hatari wa Liverpool, Luis Suarez amemkasirisha vibaya sana kocha wake Brendan Rodgers na kutuhumiwa kuwa ameshindwa kuiheshimu klabu yake na hapo jana alifanya mazoezi pekee yake ikiwa ni adhabu kutoka kwa kocha wake.
Nyota huyo raia wa Uruguay alipewa adhabu hiyo na sasa anafanya mazoezi yake na hii iantokana na maneno yake aliyotamka baada ya Liverpool kukataa ofa mbili kutoka klabu ya Arsenal.
Arsenal walituma ofa ya pauni milioni 40 na wakaongeza milioni moja ili kumsajili Suarez majira haya ya kiangazi, lakini majogoo wa jiji walikataa ofa hizo.
Saurez amemchukiza kocha wake baada ya kufanya mahojiano na magazeti mawili jumanne ya wiki hii ambapo alimtuhumu bosi wake Rodgers kushindwa kufuata ahadi yao na kushindwa kuzungumza ukweli.

Rodgers amechukizwa na tabia za nyota wake Suarez mwenye umri wa miaka 26 na amemtaka kuomba msamaha hadharani kama anataka kuichezea tena Liverpool.
Arsenal ni klabu pekee ambayo inamtaka Suarez, ngome ya mabao Anfield, lakini bado majogoo hao wa jiji wanatia ngumu kumuuza kwa wapinzani wao.

0 comments:
Post a Comment