Tuesday, August 6, 2013


IMG_1946Na Gladness Mushi , Arusha
CHAMA  cha wakulima na wafugaji kwa kanda yakaskazini(TASO) kimepewa changamoto ya kufanya tathimini juu ya ubora wa maonesho hayo kwa miaka kumi iliyopita kwa malengo ya kujua kama yana faida au hasara kwa kanda ya kaskazini kwani huenda maonesho yakatumia gharama kubwa lakini isiweze kuwasaidia wananchi.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara  Elasto Mbwilo wakati akifungua rasmi maonesho ya wakulima na wafugaji kwa kanda ya kaskazini mapema jana jijini Arusha.
Alisema kuwa kwa sasa wapo baadhi ya washiriki wanaoshiriki kimazoea ili waweze kuonekana na wao wameshiriki tu huku hata wale wanaopewa zawadi nao wakipewa zawadi na kisha kuchekelea  tu jambo ambalo Taso wanatakiwa kuangalia tathimini hiyo.
Aliongeza kuwa endapo kama chama hicho kitafanya tathimini nakuhakikisha kuwa kinawafutilia washindi wa miaka ya nyuma na sasa
basi wataweza kuwa mfano mzuri wa kudumisha Kilimo kwanza hasa kwa Mikoa ya kanda ya kaskazini na wala sio kushiriki kwa mazoea ili nao waonekane wameshiriki.
Alifafanua kuwa Chama hicho ndicho chenye msingi pekee wa kuweza kukuza na kuimarisha Kilimo kwanza na pia wanatakiwa kuhakikisha kuwa wananazia maonesho kuanzia ngazi yha chini na kuelezea jamii jinsi kutumia vema Kilimo kwanza kwa ajili ya kujikomboa na  Baa la njaa ambalo ni kikwazo kikubwa sana kwa jamii
“Nimeona maonesho mengi sana na hata hapa  nane nane wapo watu na Halmashauri ambazo wanafanya kama mazoea
tu na lengo likiwa halifikiwi sasa ninyi Taso nawasihi sana msifanye maonesho haya kama mazoea na sifa ili nanyi muonekane kama mmefanya maonesho  bali fanyeni maonesho haya kwa ajili ya kuweza kuwasaidia wakulima hata kama baadhi yao hawakushiriki katika maonesho haya basi waweze kujua jinsi watakavyoendeleza kilimo kwanza nah ii itasaidia kuongeza uzalishaji mzuri” aliongeza Mbwilo

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video