Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsindikiza Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza, wakati akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo, Agosti 29, 2013 baada ya kumaliza mapumziko yake ya siku tatu nchini. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza, wakati akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo, Agosti 29, 2013 baada ya kumaliza mapumziko yake ya siku tatu nchini. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na viongozi wengine, wakimuaga Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza, wakati akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo, Agosti 29, 2013 baada ya kumaliza mapumziko yake ya siku tatu nchini. Picha na OMR
Rais wa Burundi, Piere Nkurunzinza, akiagana na baadhi ya maofisa wa Ofisi ya Makamu wa Rais, waliofika uwanjani hapo kumsindikiza leo Agosti 29, baada ya Rais huyo kumaliza mapumziko yake ya siku tatu nchini. Kushoto ni Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal. Picha na OMR

********************
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo Alhamisi Agosti 29, 2013 amekutana na Rais Pierre Nkurunzinza katika hoteli ya Hilton Double Tree na kufanya naye mazungumzo. Rais Nkurunzinza alikuwa nchini kwa siku tatu kwa mapumziko na ameelezea kufurahishwa kuwapo Tanzania na akaeleza kuwa Tanzania na Burundi ni nchi zenye uhusiano wa kipekee na kwamba uhusiano huo umekuwepo na utaendelea kuwepo kwa miaka mingi ijayo.
Kwa upande wake Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal alimueleza Rais Nkurunzinza furaha yake kwa yeye kuchagua Tanzania kuwa sehemu ya mapumziko yake na familia yake na kwamba Tanzania inazo fursa nyingi za kitalii hali ambayo imewafanya viongozi wa nchi mbalimbali kupenda kuja hapa. Makamu wa Rais alimtakia safari njema Rais Nkurunzinza na kumueleza kuwa uhusiano wa nchi zetu unatufanya kuwa ndugu hivyo anakaribishwa tena hapa nyumbani Tanzania.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais Agosti 29, 2013, Dar es Salaam
0 comments:
Post a Comment