Friday, August 9, 2013


Na Baraka Mpenja 
Wekundu wa msimbazi Simba, kesho wanatarajia kufanya tamasha lao la “Simba Day” katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ili kuwakutanisha mashabiki, wanachama, viongozi na wachezaji wa timu yao inayojiandaa kukipiga michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara inayotarajia kuanza kutimua vumbi agosti 24 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage ameiambia MATUKIO DUNIANI kuwa maana ya Siku ya “Simba Day” ni kuwakutanisha wanachama na wapenzi wa  simba ili wapate burudani na kufurahi.
“Maana ya Simba day ni kuwakutanisha wanachama na wapenzi wa Simba ili wapate burudani na kufurahi,  hivyo  nawaomba mashabiki kufika kwa wingi uwanjani na sisi viongozi tutajitahidi sana kuwapatia kile wanachohitaji kwani tutajitahidi kuwatumia wachezaji wote waliopo”. Alisema Rage.
DSC05491Hata hivyo, Rage alisema wamepata matatizo ya wachezaji wawili kutoka Burundi,  Gilbert Kaze na Amis Tambwe  ambao hawana  uhakika wa kuwepo kutokana na matatizo ya usafiri wa ndege na mambo ya kiufundi, lakini wanajitahidi kuhakikisha kesho wanadinga hao wanawahi ili wanachama na wapenzi wao wawaone.
MASHABIKISIMBARage amesema kesho unawaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi katika tamasha la Simba Day
Kwa upande wa kikosi cha Simba, kocha msaidizi wa klabu hiyo, Jamhuri Kiwhelo “Julio”, amesema wachezaji wote wapo salama na wanajiandaa katika mchezo wa kesho dhidi ya miamba ya soka la Uganda, Sports Club Villa, majogoo wa Kampala.
“Tunashukuru Mungu mwingi wa rehema, wachezaji wote wanaendelea vizuri na wana morali ya kupambana na Sports Club Villa ya Uganda hapo kesho, hakika burudani itakuwa nzuri sana, lakini tuendelee kumuomba mungu ili kesho tucheze kwa amani”. Alisema Julio.
Pia Julio amewashukuru mashabiki wao kuendelea kuwaunga mkono katika kipindi hiki cha maandalizi  licha ya kufungwa mechi za majaribio, hivyo amewaomba kujitokeza kwa wingi hapo juu.
Katika kusherehesha tukio hilo, wasanii maarufu kama vile Juma Nature, Tunda Man na Snura ‘Mama Majanga’ watatumbuiza uwanjani hapo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video