Thursday, August 29, 2013

chaleKocha wa Tanzania Prisons, Jumanne Chale katika mechi za nyuma (Picha na Maktaba)
Na  Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Mbeya
MAAFANDE wa jeshi la Magereza, Tanzania Prisons maarufu “Wajelajela” wamesikitishwa na kufanya vibaya mechi mbili za kwanza ligi kuu soka Tanzania bara, lakini wamekiri chanzo cha kilio chao ni kukosa uzoefu kwa  mlinda mlango wao namba mbili Ibrahim Shaban baada ya kipa namba moja, Mweta kuumia na kusababisha kufungwa kirahisi, huku nao mabeki wakicheza chini ya kiwango.
Prisons alianza ligi kwa kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani, na hapo jana katika dimba hilo walilala kwa bibi kwa kufungwa  mabao 3-0 mbele ya JKT Ruvu na sasa wapo mkiani mwa msimamo wa ligi kuu.
Kocha wa klabu hiyo, Jumanne Chale amesema amekaa chini na kutathimini hali ya kikosi chake na sasa anafuta makosa ya vijana wake kabla ya kuwavaa wakali wa Tang, Coastal Union mnamo septemba 14 mwaka huu uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga, “waja leo waondoka leo”, ambao hapo jana waliwabana Yanga kwa kutoka sare ya 1-1.
Chale ameongeza kuwa kupoteza mechi mbili za mwanzo sio kwamba wamepotea, bali kuna mechi nyingi sana zinazokuja, hivyo wanajipanga upya kwa kuanzia na mechi ya wagosi wa Kaya.
“Mashabiki weye roho nyepesi wanaona kama hatuwezi, nawakumbuka mashabi wetu wa Mbeya kuwa tuna nafasi ya kujipanga vizuri, na waondoe shaka kwani tumekaa chini na kuangalia namna ya kuimarisha kikosi”. Alisema Chale.
Naye katibu mkuu wa klabu hiyo, Sadick Jumbe amesema kwa sasa timu itaendelea kuwepo Magereza ya Ukonga jiini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa Coastal Union na kikosi kitaondoka septemba 10 kuelekea Tanga.
“Kikosi kipo salama, tumepoteza mechi, lakini ni kawaida sana katika soka, sio muda muafaka wa kukata tama, bado tunao muda mzuri wa kusahihisha makosa na kufanya mambo makubwa sana”.Alisema Jumbe.
Jumbe amesema kuburuza mkia kwa mechi mbili tu si kigezo cha kuwaona maboya msimu hu, bali wanajipanga vikali mno kuhakikisha wanawapa shughuli nzito wapinzani katika mechi zijazo.
Msimu uliopita Tanzania Prisons ilimaliza katika nafasi ya 9 na ilipigana sana kukwepa mkasi wa kushuka daraja, na msimu huu mpaka sasa wanaburuza mkia kwa kutokuwa na pointi yoyote kibindoni.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video