Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportmail
KLABU ya Arsenal haina jinsi, lazima isajili sasa baada ya kupata pigo kubwa kutokana na taarifa kuwa mshambuliaji wake, Raia wa Ujerumani, Lukas Podolski atakaa nje ya uwanja kwa wiki 10 kutokana na kupata majeruhi ya nyama za paja.
Podolski, alifunga mabao mawili katika ushindi wa Arsenal wa mabao 3-1 dhidi ya Fulham jumamosi iliyopita, pia aliwainua washika bunduki hao kutoka kaskazini mwa London, katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Fenerbahce mapema wiki hii.
Vipimo vimeonesha kuwa Podolski sasa atakaa nje ya dimba kwa muda mrefu akitibiwa, na hali hii imemchanganya kocha Wenger anayetaka kuimarisha kikosi chake.
Balaa kwa Arsenal: Lukas Podolski atakaa nje ya uwanja kwa wiki 10 akibiwa majeruhi ya nyama za paja
Akizungumzia mechi ya ugenini dhidi ya Tottenham jumapili ya wiki hii, Wenger alisema: ‘Ni taarifa mbaya kuhusu Lukas Podolski kwani atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 8 hadi 10″.
Alipiga mawili: Podolski alitia kambani mawili wiki iliyopita dhidi ya Fulham
Presha ni kubwa: Arsene Wenger amekuwa akishauriwa kusajili sura mpya Emirates
Hata hivyo, Wenger anapenda wachezaji wake wote majeruhi wawe salama kuelekea dabi ya LONDON dhidi ya Tottenham.
Kiungo Mikel Arteta na nahodha Thomas Vermaelen wanaendelea kuimarika
Wenger aliongeza kuwa Arteta anaendelea vizuri, lakini anahitaji wiki chache zijazo ili kumtumia. Thomas Vermaelen anaweza kurudi uwanjani baada ya mapumziko ya kimataifa.
0 comments:
Post a Comment