Friday, August 9, 2013

SONY DSCNa Baraka Mpenja 
Mipango ya mazoezi ya maafande wa JKT Ruvu wenye makazi yao mkoani Pwana kujiandaa na ligi kuu soka Tanzania bara imevurugika baada ya nusu ya wachezaji wa kikosi kuondoka nchini kwenda nchini Kenya na Zimbabwe kushiriki mashindano ya majeshi.
Akizungumza na Mtandao wa MATUKIO DUNIANI , Kocha wa maafande hao, Mbwana Makata amesema amepata athari kwani amebaki na wachezaji wachache ikizingatiwa ni wakati wa maandalizi ya kupata kikosi cha kwanza, lakini hakuna jinsi kwani wameenda katika majukumu ya kikazi na ina umuhimu wake.
“Wachezaji wangu wanatarajia kurejea nchini kati ya Agosti 15 na 16 watakapomaliza michezo hiyo, wakifika nitakaa nao pamoja na kuandaa kikosi cha kwanza, na baada ya hapo nitatafuta mechi angalau mbili au tatu kabla ya kuanza kucheza mechi za ligi kuu”. Alisema Makata.
Makata alisema cha msingi ni kujipanga ili kufanya vizuri msimu ujao na kufanikisha malengo yetu taofauti na msimu uliopita ambapo timu ilinusurika kushuka daraja.
“Kila mtu anatakiwa kutimiza majukumu yake kama ilivyo kawaida, endapo wachezaji watazingatia maelekezo yangu, nina uhakika tutafanya vizuri zaidi msimu ujao”. Alisema Makata.
JKT Ruvu wataanza kutupa karata yao ya ligi kuu soka Tanzania bara Agosti 24 mwaka huu katika dimba la Mkwakwani jijini Tanga dhidi ya Mgambo Shooting.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video