Saturday, August 10, 2013


Nsajigwa
Na Baraka Mpenja 
Klabu Ya Lipuli ya Iringa inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara imejipanga kuwekeza katika soka la vijana ili kujijengea utamaduni wa kuepusha matumizi makubwa ya fedha kusajili wachezaji wapya.
Akizungumza na mtandao wa MATUKIO DUNIANI Kocha wa klabu hiyo, Shadrack John Nsajigwa Mwandemele amesema tangu awasili huko kikosi chache kinaendelea vizuri na mazoezi, lakini anajipanga kuwekeza katika soka la vijana.
“Kwa sasa soka linahitaji vijana zaidi, lakini kuwekeza soka hilo kunahitaji pesa zaidi, tatizo la timu zetu nyingi hazina hela, hivyo inakuwa ngumu kuetekeleza mipango”. Alisema Nsajigwa.
Kocha huyo ambaye alikuwa beki wa kushoto wa muda mrefu wa klabu ya Yanga na nahodha wa Taifa Stras, alisema programu za vijana zinahitaji muda mrefu na uvumulivu.
“Unajua huwezi kusema anaweza kumuendeleza kijana kwa miezi mitatu, unahitaji kuwa na muda angalau miaka mitatu kupata zao unalohitaji, hivyo inahitaji viongozi na mashabiki wawe na uvumilivu sana”. Alisema.
Pia Nsajigwa amepingana na watu wanaosema Tanzania haiwezi kuendelea kisoka kutokana na wachezaji wake kuwa na maumbile madogo, bali amesema wachezaji waliopo licha ya kuwa na maumbo hayo wanaweza kufanya vizuri.
Kocha huyo alisema kuna wachezaji wana maumbile madogo duniani na wanaweza kufanya kazi nzuri na kujipatia umaarufu mkubwa, kikubwa ni kujiandaa kwa nguvu na kuwekeza zaidi katika mazoezi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video