Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge(kushoto) akisikiliza taarifa kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya TAMESA ,Masel Magesa (kulia) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea leo Kivuko cha Kigamboni kuangalia kuona mfumo mpya wa ukatishati tiketi. Kivuko hicho kinasafirisha zaidi ya watu 50 elfu kwa siku.(Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Mweka Hazina wa Kivuko cha Kigamboni Juliet Julius(kushoto) akimuonyesha Naibu Waziri wa Ujenzi ,Mhandisi Gerson Lwenge(mwenye suti) jinsi ya mfumo mpya wa ukatishaji wa tiketi katika Kivuko hicho leo jijini Dar es Salaam. Mfumo huo umeboresha ukataji wa tiketi naumesaidia kupunguza msongamano pamoja na kuongezeka kwa makusanyo kuliko awali .Pichani (alievaa gauni la kitenge) ni Mtendaji Mkuu waMamlaka ya TAMESA , Masel Magesa, (kulia) Mkuu wa Kivuko cha Kigamboni Charles Irege.(Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.)
Mkuu wa Kivuko cha Kigamboni Charles Irege(alienyanyua mkono) akimpa maelezo Naibu Waziri wa Ujenzi Eng, Gerson Lwenge (mwenye suti) eneo wanalopitia wananchi baada ya kupata tiketi zao na kuelekea kupanda kivuko cha Kigamboni leo.Pichani mwenye kitenge ni Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya TAMESA , Masel Magesa.(Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO)
Mkuu wa Kivuko cha Kigamboni Charles Irege (mbele aliesimama kulia) akionyesha mfumo mzima mpya wa ukatishaji wa tiketi leo kwa Mh, Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge (kulia) pamoja na baadhi ya waandishi wa habari . Mfumo huo umepunguza msongamano kwa wanachi wanaotumia kivuko hicho na kufurahia huduma nzuri ziinazotolewa na serikali ya Tanzania
Baadhi wa wananchi wakisubiri kivuko baada ya kukata tiketi zao Leo jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment