Thursday, August 29, 2013


Pic 4 (1)
Mzee Kingunge Ngombale Mwiru
Na Hussein Makame, MAELEZO
MWANASIASA mkongwe nchini na Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kingunge Ngombale Mwiru amewataka Watanzania wasikubali kuyumbishwa kama nchi kuhusu umoja wa kitaifa, udugu na mshikamano na amani na utulivu wakati wa mchakato wa kutoa maoni ya kuunda katiba mpya.
Kingunge alitoa angalizo hilo kwenye mkutano wa kufunga rasmi mabaraza ya katiba yaliyo chini ya Chama cha Watabibu wa Tiba Asili (ATME) uliofanyika mjini Bagamoyo juzi.
Mwanasiasa huyo alitoa angalizo hilo baada ya kueleza kuwa kuna baadhi ya watu wakiwemo wanasisasa kutoa maoni ya kuunda katiba mpya yanayolenga kuvuruga umoja wa kitaifa, udugu na mshikamano na amani na utulivu.
Alisisitiza kuwa kwa sasa Tanzania umoja wa kitaifa tumeshika pazuri, kwenye udugu na mshikamano tumeshika pazuri, lakini kwenye utulivu na amani hali si nzuri sana baada ya kujitokeza watu wanaotaka kuuchafua.
“Kwa hiyo nasema iko kazi ya kufanya lazima tuendelee kuweka msimamo, tusikubali kuyumbishwa kama nchi, kwenye umoja wa kitaifa tumeshika pazuri, kwenye udugu na mshikamano tumeshika pazuri, kwenye utulivu na amani tumeshika pazuri ingawaje wenyewe sasa hivi tunachafua” alisema Kingunge.
Alifafanua kwa kuwataka Watanzania watoe mawazo ya kujenga na sio mawazo ya kuwagawanyisha Watanzania na kuwafanya waishi katika maisha yatakayoliangamiza taifa miaka ijayo.
Alisema kuwa kuna mwanasiasa mmoja visiwani Zanzibar amesema kuwa Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar mzee Karume alitishwa ndio maana akakubali kuunda muungano huo, jambo ambalo si kweli.
Akizungumzia tiba asili, Kingunge alikitaka ATME kwanza wajenge uhalali wa shughuli zinazofanywa na wanachama wake kwa kuanza kupiga vita upotoshaji wa wale ambao si watibabu wa tiba asili.
“Kupiga vita upotoshaji ni pamoja na kutazama, kufuatilia vitendo vya wanachama wenu kwa sababu wanaweza kuwa sehemu ya upotoshaji kama wanakosa uadilifu wa shughuli za tiba asili na kuingiza mazingaombwe na mambo ambayo ni ya usanii” alisema Kingune.
Aliongezakuwa kuwa tiba asili zipo na hazihitaji kupotoshwa na watabibu wa tiba hizo wanaoendesha kwa kuchanganya na ramli kwani tiba asilia ya kweli na ujanja ni upotoshaji.
Aliwashauri ATME na wanachama wake kujikita katika kufanya utafiti wa tiba mbalimbali na kutafuta ukweli juu ya mambo mbalimbali kwani kwa kufanya hivyo watapata maarifa mengi ya kuwasaidia kutoa tiba kwa uhakika.
Akisoma risala ya ATME, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Othman Shem alisema katika mabaraza ya katiba yaliyoandaliwa chini ya chama hicho, wameshirikisha mikoa 25 na wilaya 133.
Alitaja baadhi ya mambo yalipendekezwa kwenye mabaraza hayo kuwa ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaje tiba asili kuwa ni huduma ya siha, haki za binadamu liwe suala la muungano na rasilimali za taifa ziwe za Muungano.
Mabaraza hayo ya katiba chini ya ATME yalianza mikutano yake mwishoni mwa mwezi uliopita na baada ya kufunga mabaraza hayo, chama hicho kinawasilisha maoni yao leo Agosti 30 kwenye tume ya Mabadiliko ya Katiba

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video