Wednesday, August 14, 2013

1.Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani (aliyesimama) akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara katika mkutano ulioitishwa na Tume ili kuijadili na kuitolea maoni Rasimu ya Katiba Mpya wakati wa mkutano uliofanyika Wilayani humo hivi karibuni. Kulia ni Mjumbe wa Tume, Bw. Yahya Msulwa.
2.Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmshauri ya Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya, Bw. Tata Kibona akiwasilisha maoni ya wajumbe wenzake waliojadili eneo la maadili katika Rasimu ya Katiba Mpya iliytotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika hivi karibuni.
3.Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Salma Maoulidi (kulia) akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Kilimanjaro katika mkutano ulioitishwa Tume wa kuijadili na kuitolea maoni Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume hiyo. Kushoto ni Mjumbe wa Tume, Profesa Mwesiga Baregu.
………………………………………………………………………..

TUME ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwakumbusha wananchi kuwa mwisho wa kupokea maoni kuhusu Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa asasi, taasisi, na makundi ya watu yenye malengo yanayofanana ni siku ya Jumamosi, tarehe 31 Agosti 2013.
Tarehe 31 Agosti, 2013 ilipangwa na kutangazwa katika Mwongozo Kuhusu Mabaraza ya Katiba ya Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu Wenye Malengo Yanayofanana uliotolewa na Tume na ulianza kutumika tarehe 01 Juni 2013.
Utaratibu wa Kuwasilisha Maoni
Kwa mujibu wa Aya Na. 4.0 ya mwongozo huo, Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu wenye Malengo yanayofanana yanatakiwa kuwasilisha kwa Tume maoni hayo kwa njia ya randama, barua, andiko au muhtasari wa makubaliano, n.k.
Hivyo basi Asasi, Taasisi au Makundi ya watu wenye Malengo yanayofanana yanaweza kupeleka maoni yao moja kwa moja katika ofisi za Tume zilizopo jijini Dar es Salaam, Mtaa wa Ohio au Zanzibar, Mtaa wa Kikwajuni, Gofu Jengo la Mfuko wa Bararabara. Aidha, wanaweza kutuma maoni hayo kwa kutumia barua pepe ambayo ni [email protected] au anuani zifuatazo:
    1. Tume ya Mabadiliko ya Katiba, S.L.P. 1681, Dar es Salaam; au
    2. Tume ya Mabadiliko ya Katiba, S.L.P. 2775, Zanzibar.
    Muda wa Kuwasilisha Haujaongezwa
    Tume inapenda kusisitiza kuwa muda wa kupokea maoni kuhusu Rasimu ya Katiba haujaongezwa na kuwa Asasi, Taasisi na Makundi ya watu wenye Malengo yanayofanana kuzingatia tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maoni iliyopangwa na Tume.

    0 comments:

     
    voyeur porn porn movies sex videos hd porno video