Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho amesema anataka kurudisha upya familia ya wana Chelsea ambayo ilivunjika baada ya kocha aliyeondoka Rafa Benitez kumrithi kocha kipenzi cha mashabiki Roberto Di Matteo na kusababisha tofauti kwa mashabiki wa klabu hiyo.
Chelsea waliingia katika vita ya wenyewe kwa wenyewe baada ya kumfukuza kocha aliyewapa ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya, na hata baada ya Benitez kushinda kombe la Uropa haikumnusuru kufungashiwa virago.
Na mmiliki Roman Abramovich alimgeukia tena kwa mara ya pili Mourinho majira haya ya kiangazi na amefanikiwa kumrejesha.
Kocha huyo mwenye Umri wa miaka 50, raia wa Ureno aliliambia gazeti la The Sun: “Nawataka kuwa nasi kama familia ya Chelsea-familia ambayo kwa muda fulani mwaka jana ilionekana kuvunjika”.

“Nataka kuwaweka familia moja tena, kwahiyo nahitaji watuunge mkono sisi”
“Nataka wachezaji waungwe mkono, nawataka kuiunga mkoa Chelsea”
“Nawata kutuunga mkono wakati wa shida raha, tukiwa nyumbani na ugenini, tunaposhinda na kushindwa”
Kupoteza sio kawaida kwa Mourinho na sio neno lake, ni kitu ambacho hataki kitokee na hataki kuzungumzia sana”


0 comments:
Post a Comment