Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho amemshutumu mwamuzi wa mchezo wa jana, Jonas Eriksson kuwa aliua matumaini ya klabu yake kutwaa kombe la UEFA Super Cup — baada ya Romelu Lukaku kukosa mkwaju wa penati uliompa kocha Pep Guardiola wa Bayern Munich ubingwa kwa changamoto yamikwaju penati 5-4.
Eriksson alimtoa kwa kadi nyekundu , Ramires baada ya kufanya madhambi mara mbili na hivyo kuilazimu Chelsea kucheza dakika tano za mwisho na muda wa nyongeza wakiwa 10 uwanjani.
Kakosa mzigo: Mourinho akiangalia chini baada ya mchezo kumalizika, lakini amemtupia lawama mwamuzi wa mchezo huo
Endelea mbele: Guardiola ameendelea kuwa mbabe kwa Mourinho
Mourinho alisema: “Nimevunjika moyo kwa sababu timu bora imepoteza. Timu ambayo kwa asilimia kubwa ilistahili ushindi, imepoteza. Lakini katika mpira wa miguu mambo haya hutokea”.
“Ukiniuliza mimi kwa sheria, sheria kwa sheria, ndiyo ilikuwa kadi ya pili ya njano. Lakini huwezi kuamua maamuzi kama yale kwa kila tukio la vile”.
“Refa mzuri wa soka la Uingereza angesimamisha mpira na kumwambia Ramires, “Kuwa makini, usimuumize mtu, lakini usirudie tena kufanya hivyo”. Alikuwa anawaambiwa wachezaji wa Bayern, “Msicheze rafu, msiwe na jaziba. Chezeni mchezo wa haki”. Alisema Mourinho.
Amepoteza: Lukaku akiangalia kwa uchungu baada ya kukosa mkwaju wa penati
0 comments:
Post a Comment