Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
KOCHA wa Chelsea, Mreno, Jose Mourinho ameunga mkono kauli ya kocha Alan Pardew ambaye ametaka dirisha la usajili liwe linafungwa kabla ya kuanza msimu mpya.
Kocha huyo wa paka Weusi, Newcastle, Pardew, amechukizwa na kitendo cha Arsenal kuendelea kumshawishi kiungo wake Yohan Cabaye ili wamsajili, hivyo ametaka dirisha liwe linafungwa kabla ya kuanza mechi za kwanza za ligi kuu ili klabu pinzani kuacha kuwachanganya wachezaji wa timu nyingine.
Na sasa kauli hiyo iliyoungwa mkono na Mourinho itakuwa na maana Old Trafford, kwani bosi huyo wa Chelsea anamuwinda mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney – kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
“Hakuna kilichobadilika, kiukweli naungana na Pardew kuwa dirisha la usajili linachelewa kufungwa, hadi mechi ya tatu na nne ndio linafungwa, hapana”. Alisema Mourinho.
Kakubali: Jose Mourinho amesema dirisha la usajili linachelewa kufungwa baada ya msimu mpya wa ligi kuanza
Shangwe tu: Mourinho aliinuka kutoka katika benchi na kushangilia bao la Frank Lampard alilofunga kwa mpira wa adhabu dhidi ya Hull City jumapili wa wiki iliyipita
Mourinho bado anaendelea kuiwinda saini ya Rooney, lakini ofa yake ya pauni milioni 40 ilitupiliwa mbali na kocha wa United, David Moyes alisema nyota wake hauzwi.
Anawindwa : Wayne Rooney, aliichezea Manchester United katika mechi dhidi ya Swansea ya Michu, lakini bado anawindwa na Chelsea
0 comments:
Post a Comment