Tuesday, August 13, 2013


PIC 2Na Gladness Mushi wa Fullshangwe-Manyara
Mwenyekiti wa Mtaa wa Sekondari, Mji mdogo wa Mirerani Wilayani
Simanjiro Mkoani Manyara, Hussein Msokoto (CCM) amechaguliwa tena kuwa
Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka ya mji huo.
Katika uchaguzi huo uliofanyika juzi, Msokoto ambaye hakupata upinzani
kutoka Chadema wenye wajumbe wawili, alipata kura 11 za ndiyo na mbili
za hapana ambapo mjumbe mmoja hakupiga kura yake.
Akizungumza wakati alipotangazwa na Ofisa Tarafa ya Moipo, Joseph
Mtataiko kukalia tena kiti hicho, Msokoto aliwashukuru wajumbe hao kwa
kumchagua tena kushika nafasi hiyo na aliwaahidi ataendelea kutoa
ushirikiano kwao.
“Kupitia nafasi hii napenda kuwahakikishia kuwa nitaendeleza juhudi
zangu zote za kujenga Mirerani tukishirikiano wote kwa pamoja na pia
tuendeleze ushirikiano katika kusukuma mbele gurudumu la mji wetu,”
alisema Msokoto.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mamlama ya mji huo, Albert Siloli
aliwatangaza wajumbe wa kamati ya Fedha kuwa ni Justin Nyari, Edith
Momo, Hussein Msokoto, Joseph Masasi na Ombeni Olesang’enoi.
Nao, Wajumbe wa kamati ya ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, Benedict
Shayo, Sophia Wawa, Justin Nyari, Aurelia Michael na Primy Shirima
walimchagua Joseph Masasi kuwa Mwenyekiti wao.
Wajumbe wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji, Wilbert Nyari, Said Kuzecha,
Abdon Casmir, Kaanael Minja na Rachel Kinariki, walimchagua Ombeni
OleSang’enoi kuwa Mwenyekiti wa kamati hiyo.
Kamati ya Ukimwi inaundwa na Hussein Msokoto, Isack Mgaya, Lucas
Zacharia, Edith Momo, Jovin Rweyemamu, kijana mmoja, kiongozi wa dini
ya kikristu mmoja na kiongozi wa dini ya kiislamu mmoja

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video