Na Gervas Charles Mwatebela, Dar es salaam
Imeelezwa kuwa misaada ya wahisani itakuwa na tija endapo nchi zinazoendelea kiuchumi zitakuwa makini kutumia fedha zake kama zilivyokusudia.
Akizungumza wakati wa mkutano wa kujadili misaada ya kibajeti inayotolewa na jumuiya ya ulaya kwa Tanzania katibu mkuu wa hazina Penieli Lyimo amesema kuwa kwa sasa watadhibiti mianya ya upotevu wa fedha.
Bwana Lyimo amesema kuwa misaada inayotolewa na wahisani ni muhimu kwa maendeleo ya sekta mbalimbali za huduma za jamii ikiwemo elimu,afya na nyinginezo.
Naye Naibu mtendaji mkuu wa jumuiya akishughulikia misaada hiyo Bi.Maria van Berlekom amesema anaamini wakati sasa umefika wa kuketi pamoja na kutathmini matumizi ya misaada na namna ya kupata mafanikio zaidi ya kibajeti.
0 comments:
Post a Comment