Friday, August 30, 2013

RC AKIFUNGUA KIKAOMkuu wa Mko wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe akifungua kikao cha Waganga, Maafisa Afya na wataalam wengine wa Masuala ya Lishe wakimsikiliza katika kikao cha kujadili namna ya kuboresha lishe na kutokomeza utapiamulo Mkoani KATAVI.
MTOA MADA MR MDAHAMwezeshaji kutoka wizara ya Afya na ustawi wa jamii kutoka kitengo cha lishe Frasins Mdaha akitoa mada kwa watalaam wa lishe mkoani Katavi.
waganga wa mkopa wa kataviWashiriki wa Kikao cha kuboresha masuala ya Lishe ili kupunguza nap engine kutokomeza kabisa utapiamulo mkoani  Katavi ambao ni miongoni mwa mikoa iliyokumbwa na tatizo hilo.
mikambiMtaalamu wa Lishe kutoka Hospilatali ya Wilaya ya Mpanda Bi Henerika Mikambi akipokea kitabu kinachozungumzia masuala ya lishe kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe baada ya kujibu swali lililoulizwa kwa washiriki wa kikao hicho  lisemalo nini maana ya Afya likajibiwa na Mama Mikambi na kuzawadiwa Zawadi ya Kitabu .kulia kwa mkuu wa Mkoa ni Mhandisi Emanuel Kalobelo ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa KATAVI
(Picha zote na Kibada Kibada- Katavi)
Na Kibada Kibada- Katavi
Pamoja na kuongoza kwa uzalishaji wa chakula mikoa ya nyanda za juu kusini bado inaonekana kuongoza kwa utapiamulo hapa nchini ambapo kiwango cha utapiamulo kiko asilimia 42 ukilinganisha na kiwango cha kitaifa ambacho ni asilimia 50 kwa watu wenye utapiamulo.
Kwa majibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2010 huu limeonekana tatizo la utapiamolo kwa mikoa ya nyanda za juu kusini  ni kubwa zaidi kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano na akina mama wanaoendelea kuzaa.
Hayo yameelezwa na Mtaalam wa Lishe kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Taasisi ya Chakula  na Lishe Fransis Mdaha wakati akitoa mada juu ya utapia molo  kwa Waganga,Maafisa Afya,na Wataalam wa Lishe katika Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi kwenye ukumbi Idara ya Maji  Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
Mdaha ameeleza kuwa suala la utamimolo kwa Mikoa ya nyanda za juu kusini ni mkubwa sana  kwa mikoa ya Rukwa,Katavi,Njombe,Iringa Ruvuma na Mbeya hali inayoonesha kuwa kiwango hicho ni kikubwa sana ukilinganisha ni Mikoa mingine hapa nchini.
 Akifungua kikao hicho mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu amehimiza umuhimu wa ulaji wa Chakula cha kutoshereza mahitaji  ya familia, kuwaomba viongozi wa taasisi za dini kwa kusaidiana na Mkoa kuelimisha umma juu ya ulaji wa vyakula vyenye lishe bora ili kuondokana na suala la utapiamolo miongoni mwa jamii.
Alisema huwezi kufanya maendeleo bila kuwa na Afya  njema mwili kama hauna lishe ya kutosha huwezi kufanya shughuli za maendeleo.
Amesiagiza Halmashauri na Idara ya kuhakikisha Mkoa unaweka mipango yao katika bajeti kuhakikisha inawekwe kwenye bajeti zao ili kuwe namipango ya kuhamasisha suala la lishe katika Mkoa.
Alisema makundi yanayoathirika zaidi ni watoto na makundi ya wanawake wanaoendelea kuzaa hao ndio wako kwenye kundi la kuathirika na upapiamulo nakuongeza kuwa utapia mulo ni janga la kitaifa..
Naye Mwakiliishi wa kutoka Water Leeds  Nyanda za Juu Kusini Mkoani Mbeya Jamila Mwankemwa alitaja baadhi ya sababu zinazochangia kuwepo kwa utapiamulo kuwa ni pamoja na mila potofu za jamii katika mikoa hiyo ya nyanda za juu kusini,Watu kutozingatia ulaji wa chakula kwa kufuata kanuni za lishe.
Sababu nyingine ni umasikini wa kipato miongoni mwa jamii nyingi za wananchi wakazi wa mikoa hiyo na nchi kwa ujumla pamoja na sababu nyingine za Kijamii.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video