Tuesday, August 20, 2013

1 (1)Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema akiongea na Wanamichezo wa Polisi Tanzania wanaoshiriki Michezo ya nane ya Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kusini mwa Afrika  (SARPCCO GAMES) nchini Namibia wakati alipowatembelea katika hoteli waliyofikia katika jiji la Windhoek.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)
2Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema akiwasalimia Wanamichezo wa Polisi Tanzania wanaoshiriki Michezo ya nane ya Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kusini mwa Afrika  (SARPCCO GAMES) nchini Namibia wakati wa ufunguzi wa Michezo hiyo katika uwanja wa Taifa wa Namibia.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)
3Baadhi ya Wanamichezo wanaounda timu ya Polisi Tanzania inayoshiriki michezo ya nane ya Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kusini mwa Afrika  (SARPCCO GAMES) nchini Namibia wakiwa katika picha ya pamoja moja wakati wa ufunguzi wa michezo hiyo katika uwanja wa Taifa wa Namibia. (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)
4Kikundi cha Sarakasi kikitoa burudani wakati wa ufunguzi wa Michezo ya nane ya Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kusini mwa Afrika  (SARPCCO GAMES) nchini Namibia katika uwanja wa Taifa wa Namibia.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)
6Wanamichezo wa Polisi Tanzania wanaoshiriki Michezo ya Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kusini mwa Afrika  (SARPCCO GAMES) nchini Namibia wakipita mbele ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Michezo hiyo katika uwanja wa Taifa wa Namibia.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia)
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia.
Hatimaye michezo ya nane kwa majeshi ya Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO GAMES) yamefunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Namibia Dk Hage Geingob katika uwanja wa Taifa wa Namibia na kupambwa na burudani mbalimbali zikiwemo ngoma, nyimbo sarakasi na maonyesho ya helkopta. 
Ufunguzi wa mashindano hayo ulihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi wanachama wa SARPCCO akiwemo IGP Said Mwema. 
Akizungumza katika ufunguzi huo Dk Geingob alizitaka timu zinazoshiriki mashindano hayo kushindana kwa nidhamu na kudumisha urafiki uliopo ili kuweza kukabiliana na uhalifu kwa kubadilishana mbinu na mikakati kutoka katika mataifa yao kwa lengo la kuwa na ukanda salama wa Kusini mwa Afrika.
Alisema nchi zinashiriki zinahitaji ushindi lakini ni vyema zikatambua kuwa timu moja na bora ndiyo itakayonyakua ushindi kwa kuwa mshindi ni mmoja tu kati ya mataifa yote yaliyoshiriki. 
Wakati huohuo Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema amewataka wachezaji wa Tanzania kuhakikisha kuwa wanarejea na ushindi ili kupata zawadi nono ambazo amewaaandalia endapo wataibuka na ushindi katika michezo hiyo.
IGP Mwema aliyasema hayo wakati alipowatembelea  na kuzungumza na wachezaji wa Tanzania katika hoteli waliyofikia ili kuwapa hamasa na morali wakati wote wa michezo hiyo.
 
Alisema kitu kikubwa ambacho wachezaji hao wamekifuata nchini Namibia ni ushindi hivyo wahakikishe kuwa wanacheza michezo yote kwa morali na kuibuka na ushindi jambo ambalo litalitea taifa na Jeshi la Polisi  sifa.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video