Na Walter Muguluchuma-mpanda
Mbunge wa Jimbo la Mpanda mjini ambae pia ni Makamu wa mwenyekiti wa Taifa wa chama cha CHADEMA Said Amour Arfi amefanyiwa upasuaji wa nyonga Nchini India ambako alipelekwa kwa ajiri ya matibabu
Mdogo wa Mbunge huyo Nassor Arfi alisema kaka yake alifanyiwa upasuaji hapo juzi katika hospitali ya Apolo ya nchini humo baada ya kupewa rufaa kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Alisema Arfi aliondoka hapa Nchini Agosti 25 mwaka huu majira ya saa tisa alasiri kwa ndege ya shirika la India akiwa amefuatana na mkewe ambapo walifika siku hiyo hiyo na kupitiliza kwenye hospital hiyo.
Alifafanua kuwa mheshimiwa Arfi afya yake ilianza kuteteleka toka mwezi wa juni mwaka huu .
Mwihoni mwa wiki alipo pewa rufaa ya kwenda kutibiwa Nchini India
Mdogo wake huyo alisema kuwa safari hiyo ya kwenda kutibiwa Nchini India imegharamiwa na ofisi ya Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania
Alisema hari ya mbunge huyo baada ya kufanyiwa upasuaji huo wa nyonga inaendelea vizuri na kwa sasa ameanza kuongea
Mwaka 2011 mbunge huyo aliwahi kwenda nchini India kwa matibabu kama hayo mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa 2010
0 comments:
Post a Comment