Wednesday, August 28, 2013

01Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohd akizungumza na wawakilishi wa vyama vya siasa Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar juu ya suala zima la uboreshaji Sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
02Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu wa Chama cha Wananchi CUF Salum Bimani akitoa mchango wake katika mkutano ulioitishwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa pili wa Rais Ofisini kwake Vuga kwa lengo la kufanikisha Sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar
03Viongozi  wa vyama vya siasa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Muhammed Aboud Mohd alipokutana nao Ofisini kwake Vuga mjini Zanzibar.
(Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar).
Khadija Khamis  na Amina Shaibu wa Habari Maelezo Zanzibar  
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewataka  viongozi wa vyama vya siasa kushirikiana  na kutoa mchango wao wa hali na mali katika kufanikisha sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Kauli hiyo imetolewa jana  na Waziri  wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Abuod Muhammed alipokutana  na wawakilishi  wa vyama vya siasa ofisini kwa ke Vuga.
Alisema kuwa Serikali imeamua kuzifanya   sherehe hizo kuwa za aina yake na  zinahitaji mchango wa kila mtu bila ya kuangalia  itikadi ya vyama vya siasa ili  kuonyesha  uelewa wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa nchini.
“Mapinduzi yetu yanafikia nusu karne, tutafanya sherehe kubwa na tumeamua kuyashirikisha  makundi yote kuanzia hatua za awali wakiwemo  viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wafanya biasha, makampuni, taasisi binafsi,  waandishi wa habari na makundi mengine ili kufanikisha sherehe hizo,” alisema Waziri Aboud
Waziri wa Nchi Ofisi ya Mkamu wa pili wa Rais  alidokeza  kuwa Mgeni Rasmi katika Sherehe hizo atakuwa Rais wa Jamhuri ya watu wa China na wageni kutoka nchi za Afrika Mashariki, nchi wanachama wa SADC pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya ulaya pia wamealikwa kushiriki.
Aidha alisema  katika shamrashara za sherehe hizo kutakuwa na ufunguzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo, uwekaji wa mawe ya msingi,  makongamano na utajengwa mnara maalumu wa miaka 50 ya Mapinduzi  ya  Zanzibar .
Nae katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamo wa pili wa Rais Dkt Khalid Salum Muhammed alisema kuwa katika kufanikisha sherehe hizo kumeandaliwa vazi rasmi  siku ya kilele cha sherehe hizo  yenye rangi za bendera ya Zanzibar.
Aliongeza kuwa  vipindi maalum  na picha za mafanikio ya Mapinduzi katika kipindi cha miaka 50 vitaendelea kuonyeshwa  kupitia  vyombo mbali mbali vya Serikali na binafsi  na changamoto zilizojitokeza ili kuweza kukabiliana nazo katika kipindi chengine cha  miaka  50 .
 Mapinduzi ya  Zanzibar ya mwaka 1964  yaliyoongozwa na Marehemu Abeid Amani Karume yatatimiza miaka 50 tarehe 12 Januari 2014  na kilele chake kitakuwa katika uwanja wa Amaan

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video