Tuesday, August 13, 2013

LIGI DARAJA LA KWANZA MBEYA CITY NA BURKINA FC JAMHURI MORO PIX NO 1Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya inayojiandaa na mitanange ya ligi kuu Tanzania bara inayotarajia kuanza kushika kasi Agosti 24 mwaka huu imeshuka dimbani katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Maafande wa Polisi Morogoro katika uwanja wa Jamhuri na kulala kwa mabao 2-1.
Akizungumza kutoka Morogoro kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi amesema mechi hiyo ilikuwa nzuri kwake na kipimo kizuri, lakini wamefungwa kutokana na makosa yaliyofanywa na safu yake ya ulinzi.
“Bado kuna shida katika safu yangu ya ulinzi, hata safu ya ushambuliaji haijakaa sawa, ila nitajitahidi kufuta makosa hayo kabla ya kuanza kujitupa michuano ya ligi kuu”. Alisema Mwambusi.
Mwambusi amekiri kuwa msimu wa ligi kuu utakuwa mgumu sana kwao kwani ndio kwanza watashiriki kwa mara ya kwanza, lakini kwa namna wanavyoendelea kujiandaa ana matumaini ya kufanya vizuri sana.
Kwa upande wa Polisi Morogoro walioshuka daraja msimu uliopita, Afisa habari wa klabu hiyo Clemence Banzo amesema mechi hiyo ilikuwa nzuri kwako, lakini amewazungumzia Mbeya City kwamba wanahitaji muda na wanatakiwa kuongeza wachezaji wazoefu ambao wanaweza kuwasaidia kufika mbali.
“Mimi nilivyowaona wachezaji wa Mbeya City bado wanatakiwa kujipanga zaidi, wana shida katika safu ya ulinzi na ushambuliaji. Nimeongea na Meneja wa timu yao na kumshauri waongeze wachezaji wenye uzoefu”. Alisema Banzo.
Mbeya City ni miongoni mwa timu tatu zilizopanda ligi kuu Tanzania bara ambapo nyingine ni Rhino Rangers ya Tabora na Ashanti United ya jijini Dar es salaam.
Klabu hiyo yenye makazi yake jijini Mbeya itaanza kibarua cha ligi kuu kwa kucheza mechi katika uwanja wake wa nyumbani wa Sokoine dhidi ya “Wanankulukumbi”, Kagera Sugar.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video