Saturday, August 31, 2013


Na Baraka Mpenja , Mbeya
TIMU ya Mbeya City imerudisha fadhila kwa waandishi wa habari jijini  hapa na nje ya jiji kwa msaada mkubwa wanaoendelea  kutoa kwa kuitambulisha klabu hiyo kwa jamii  ya wapenda soka kupitia vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo redio, Televisheni, blogs, websites na magazeti.
Akizungumza na Mtandao wa MATUKIO DUNIANI, Afisa habari wa klabu hiyo, Fredy Jackson amesema uongozi wa klabu hiyo ambayo msimu huu wa 2013/2014 ni wa kwanza kwake kushiriki ligi kuu soka Tanzania bara, unawashukuru sana wana habari kwa jinsi walivyoshiriki kuitangaza na kuifahamisha jamii kuhusu timu hiyo.
“Ndugu wanahabari tunatambua ushirikiano wenu katika kuiendeleza timu na tunaahidi ushirikiano wa dhati na ninyi ”. Alisema Jackson
DSC00380Wachezaji wa Mbeya City wakishangilia bao la pilina la  ushindi Agosti 28 mwaka huu uwanja wa sokoine dhidi ya Ruvu Shooting
Afisa habari huyo aliongeza kwa  ushauri wa waandishi wa habari ni muhimu sana na wapo tayari kuupokea na kuufanyia kazi.
“Watu wa habari wana mawazo endelevu sana, kama wanaona kitu hakiendi sawa basi wasisite kutuambia,  sisi tunajali sana kazi yao na ndio maana tunatazama, tunasoma na tunasikiliza vyombo vya habari ili kujua maoni yao kwa timu, hivyo waandishi waendele kutuunga mkono”. Alisema Jackson.
DSC00389Mashabiki wa Mbeya City wakishangilia bao la pili na la ushindi dhidi ya Ruvu Shooting uwanja sokoinie Agosti 24 mwaka huu
Pia Jackson amewapongeza na kuwashukuru mashabiki wao kwa kutoa mchango mkubwa kwa timu, kwani siku zote wamekuwa wakijitokeza kwa wingi timu inaposhuka dimbani.
“Mshabiki wa Mbeya wamekuwa na uzalendo mkubwa sana, wanawatia moyo wachezaji na benchi la ufundi, hivyo tunawaomba kuendelea na jitihada hizo ili kufikia malengo ya pamoja”. Alisema Jackson.
Mbeya City ni timu inayomilikiwa na halmashauri ya jiji la Mbeya na kwa mara ya kwanza inashiriki ligi kuu Tanzania bara na mpaka sasa ipo nafasi ya saba katika msimamo ikiwa na pointi 4 baada ya kushinda mechi moja dhidi ya Ruvu Shooting agosti 28 na kutoka suluhu ya bila kufungana dhidi ya Kagera Sugar agosti 24 mwaka na mechi zote zilichezwa uwanja wa sokoine jijini Mbeya.
Timu hiyo iliyosheheni vijana wadogo wanaoonekana kuimarika kila siku wapo chini ya kocha Juma Mwambusi “Ferguson wa Mbeya” huku akisaidiwa na Maka Mwalwisyi.
Klabu hiyo inatarajia kushuka dimbani septemba 14 mwaka huu katika uwanja wake wa Sokoine dhidi ya Mabingw watetezi, klabu ya Yanga. Na hii itakuwa mechi ya tatu mfululizo kuchezo nyumbani.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video