Thursday, August 29, 2013


Na Baraka Mpenja, Mbeya
Hakika jana mashabiki wa soka jijini Mbeya wamewaduwaza wapenzi wa michezo hususani  kandanda nchini Tanzania kwa kitendo chao cha kumzomea kocha mkuu wa klabu ya Mbeya City, Juma Mwambusi na wachezaji wake, huku wakishinikiza ushindi katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting, na wakitoa vitisho kuwa timu ikitoa sare hapataeleweka.
Jicho la MATUKIO DUNIANI lilikuwepo katika mchezo wa jana  uwanja wa Sokoine uliomalizika kwa wenyeji kupata bao la ushindi katika dakika za lala kwa buruani ambazo hazimruhusu hata kuku kumeza punje kupitia kwa nyota wao Steven Mazanda, jezi namba nane mgongoni, huku bao la kwanza likifungwa dakika ya 7 kipindi cha kwanza kupitia kwa Paul Nonga, wakati dakika ya 25 kipindi cha kwanza Ruvu walijipatia bao kupitia kwa Shaban Susaz.
Matokeo yalikuwa mazuri kwa Mbeya City, lakini ushindi huo ulipatikana wakati mashabiki wengi wakiamini mechi inamalizika kwa sare ya bao 1-1, ila soka huwa halipigiwi hesabu kwa namna hiyo, kwani wakati wowote mambo yanaweza kubadilika kama ilivyokuwa jana.
Lakini kituko kilichooneshwa na mashabiki wa Mbeya City cha kuzomea na kuimba nyimbo za kushinikiza matokeo mazuri na kumtishia kocha Mwambusi kuwa akitoa sare hapatoshi, hakika si uungwana kabisa ukizingatia timu hiyo ni mpya na ndio kwanza ulikuwa mchezo wake wa pili.
DIGITAL CAMERAKocha wa Mbeya City Juma Mwambusi wakati akiongea na waandishi wa habari katika mchezo wa jana, hakika alikerwa na mashabiki kuzomea
Mechi ya ufunguzi walitoka sare ya timu kongwe ya Kagera Sugar, matokeo hayo yalikuwa mazuri kwani ilikuwa mechi ya ufunguzi kwao, lakini mashabiki hawakuona kuwa matokeo hayo ni mazuri na hapo jana wakawa na hisia tofauti na kuona timu yao inafanya vibaya.
Kiukweli bado ni mapema sana kuanza chokochoko kwa benchi la Ufundi, timu inatakiwa kupewa muda, na ukiangalia kwa undani kikosi cha Mwambusi ni kizuri japo kuna shida katika safu ya ushambuliaji ambapo huwa kinapoteza nafasi nyingi.
Kinachotakiwa kwa mashabiki ni kuiunga mkono timu na kocha wake kwani uwezo wa kukinoa kikosi anao na ndio maana alifanya vizuri ligi daraja la kwanza na kupanda ligi kuu.
Kama wataendelea na tabia ya kuzomea timu yenye pointi 4 katika mechi mbili, tena ni ngeni, basi watabaki kuwa wasindikizaji tu kwani soka halina hesabu za haraka kiasi hicho.
DSC00380Wachezaji wa Mbeya City walipokuwa wanashangilia bao la ushinda hapo jana (Picha na Mbeya Yetu Blog)
Baada ya mechi ya jana, kocha Juma Mwambusi alionekana dhihiri kuwa amechukizwa sana na kitendo kile na ndio maana wakati akiongea na waandishi wa habari aliweka wazi kukerwa na tabia ya mashabiki wake kuzomea timu yao.
Kimsingi Mwambusi aliongea jambo la maana kwa kuwataka mashabiki kuipa muda timu yao kwani ndio kwanza inajengwa , huku ikiwa imesheheni wachezaji vijana.
Kikubwa mashabiki waache tabia ya upuuzi kama ya jana, haipendezi kabisa na inaonekana kukosa ukomavu wa kushabikia soka, kwani wanakosa uvumilivu mapema sana.
DSC00389Mshabiki wa Mbeya City katika mchezo wa jana (Picha na Mbeya Yetu Blog)
Mbali na hilo, tatizo la mashabiki kuingia uwanjani wakati bado wachezaji wapo baada ya mechi kumalizika, ni hatari sana kwani litakuja kuleta madhara makubwa sana.
Imekuwa kawaida sana kwa maaskari kuwaacha mashibi wakiingia uwanjani wakati bado shughuli za uwajani hazijamalizika, na kama itatokea mtu ana nia mbaya ya mchezaji au mwandishi wa habari ataweza kumdhuru kirahisi na watakumbuka shuka wakati kumekucha.
Chukulia shabiki kachukizwa na mchezaji na ameingia na wembe au sindano na akaamua kumchoma wakati akishangilia ndani ya uwanja, nani atajua na nani atalaumiwa?.
Haya mambo yanatakiwa kudhibitiwa mapema na viongozi wa soka katika viwanja vya mikoani kwani ipo siku madhara makubwa yatakuja kutokea.
Jeshi la polisi linatakiwa kuwa makini sana kuimarisha ulinzi baada ya mechi kwani watakuja kulaumiwa sana wakati mambo yameshaharibika.
Tunatumaini mechi ya septemba 14 dhidi ya Yanga, mambo yatakuwa safi zaidi na ulinzi utakuwa imara.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video