Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
KOCHA mkuu wa Barcelona , Tata Martino amekanusha taarifa za kujihusisha na uhamisho wa wachezaji wawili wanaocheza ligi kuu soka nchini England, David Luiz au Daniel Agger, na kuthibitisha kuwa anafurahia wachezaji wake wa safu ya ulinzi alionao kwa sasa katika kikosi chake.
Wakatalunya wamekuwa wakihusishwa kutumia dau kubwa kuwasajili wachezaji hao wawili, ingawa klabu za Chelsea na Liverpool zimeonesha msimamo wa kutokuwauza.
Na kocha Martino katika mkutano na waandishi wa habari wakati akizungumzia mechi ya kwanza ya La Liga dhidi ya Levante amesema:m”Tunaye Puyol, Pique, Mascherano, Bartra, hata Adriano. Kama itatokea kutakuwa na majeruhi dirisha dogo mwezi januari sio mbali”


Maneno ya kocha Martino yanamaanisha makocha Brendan Rodgers na Jose Mourinho wanaweza kuendelea kuwamiliki wachezaji wao.
Rodgers amemteua Agger kuwa nahodha msaidiz ili kumshawishi kubakia Anfield, wakati huo huo Mourinho kuhusu Luiz alisema “Tunataka abakie hapa na tunajua timu kubwa kama Barcelona inajaribu kumsajili beki wa kati bora zaidi duniani, lakini kwa kuwa wakweli, hakuna nafasi ya kumuuza David Luiz “.

0 comments:
Post a Comment