Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
MAKAMU bingwa wa ligi kuu soka nchini England, Manchester City wameanza maisha mapya chini ya kocha Manuel Pellegrini kwa ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Newcastle waliocheza wakiwa pungufu baada ya Steven Taylor kupewa kadi nyekundu dakika ya 45 katika dimba la Etihad usiku huu.
Steven Taylor alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kwa mkono wake Aguero akiwa karibu na mwamuzi wa mchezo huo Andre Marriner.
Mabao ya Manchester City yamefungwa na David Silva dakika ya 6, Sergio Kun Aguero dakika ya 22, Yaya Toure dakika ya 54 na Samir Nasri katika dakika ya 74.
Kikosi cha Man City: Hart, Zabaleta, Kompany (Javi Garcia 71), Lescott, Clichy, Jesus Navas, Toure, Fernandinho, Silva (Negredo 80), Aguero (Nasri 62), Dzeko.
Wachezaji wa akiba: Milner, Kolarov, Rodwell, Pantilimon.
Waliopata kadi: Dzeko, Fernandinho.
Magoli: Silva 6, Aguero 22, Toure 50, Nasri 75.
Kikosi cha Newcastle: Krul, Debuchy, Steven Taylor, Coloccini, Yanga-Mbiwa, Sissoko, Tiote, Gutierrez (Anita 44), Ben Arfa (Sammy Ameobi 65), Cisse, Gouffran (Dummett 45).
Wachezaji wa akiba: Elliot, Marveaux, Shola Ameobi, Obertan.
Kadi nyekundu: Steven Taylor (45).
Kdi za njano: Yanga-Mbiwa, Sissoko, Debuchy.
Mashabiki: 46,842
Mwamuzi: Andre Marriner (W Midlands).
Nipe tano jembe! Yaya Toure na David Silva wote wamefunga katika mchezo wa leo dhidi ya Newcastle
Hamuwezi, mimi fundi: Fabricio Coloccini na Tim Krul wakiwa hawana la kufanya wakati mpira wa kichwa uliopigwa na Silva ukitikisa nyavuni
Hesabu mbovu: Sliva (kulia), bao lake la kwanza ligi kuu England amefunga kwa kichwa msimu wa 2013/2014
Bao la pili: Sergio Aguero alipiga shuti kali na kuifungia Manchester City bao la pili katika dakika ya 22
Karuka juu mno: Aguero akishangilia bao lake
Kadi nyekundu: Steven Taylor alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi Aguero mwishoni mwa kipindi cha kwanza
Bao la nne: Samir Nasri alimaliza kazi dakika ya 75
0 comments:
Post a Comment