Saturday, August 31, 2013

DSC00559Mchezaji wa timu ya soka ya Simba SC ya jijini Dar es salaam, Edward Christopher, akipatiwa
huduma ya kusuguliwa kwenye saluni ya kisasa ya Nick Babershop ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, baada ya mchezo wa kirafiki uliofanyika juzi Simba ilishinda bao 1-0
DSC00557Mchezaji wa timu ya soka ya Simba SC ya jijini Dar es salaam, Edward Christopher, akipatiwa huduma ya kusuguliwa kwenye saluni ya kisasa ya Nick Babershop ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, baada ya mchezo wa kirafiki uliofanyika juzi Simba ilishinda bao 1-0
DSC00545Mkuu wa kituo cha polisi Mirerani, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, SP Ally Mohamed Mkalipa, akisalimiana na Abdulhalim Humudi, wakati akiikagua timu ya Simba ilipocheza juzi na timu ya Tanzanite FC, baada ya kutembelea machimbo ya madini ya Tanzanite.
Picha na  woinde shizza, Mererani
……………….
Na Woinde Shizza,Manyara
Timu ya soka ya Simba SC ya Jijini Dar es salaam jana imetembelea machimbo ya madini ya Tanzanite ambapo hapa duniani yanapatikana peke yake Mji mdogo wa Mirerani, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Wachezaji hao wakiongozwa na viongozi wao Makamu Mwenyekiti, Joseph Itangire (Mzee Kinesi) na
kocha mkuu Abdalah Kibadeni, walitembelea kampuni ya TanzaniteOne na kujionea namna shughuli za uchimbaji zinavyofanyika.
Hata hivyo, wachezaji hao wakizungumza kwenye machimbo hayo ya madini ya Tanzanite, walisema
hiyo ni mara yao ya kwanza kutembelea machimbo hayo kwani awali walikuwa wanasikia Tanzanite katika vyombo vya habari pekee.
Walipotembelea machimbo hayo pia walicheza mchezo wa kirafiki na timu ya Tanzanite FC inayomilikwa na Jofrey Nyigu (Mnyalu) na wakaifunga bao 1-0 lililotiwa kimiani na mshambuliaji wao hatari Abdalah Seseme.
Seseme alifunga bao hilo baada ya kupewa pasi na Ramadhan Singano “Messi”
aliyewachambua mabeki wa Tanzanite FC, Elibariki Bryson na Abdilahi Yusuph walioshindwa kumpa
ulinzi kipa wao Achibald Kileo.
Baada ya kumalizika mchezo huo wa kirafiki, timu ya Simba ilikwenda kwenye saluni ya kisasa ya Nick Baber shop iliyopo Mirerani na kufanyiwa huduma ya kuchuliwa misuli, kuoga, kusuguliwa uso,miguu na kunyolewa nywele.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video