Na Baraka Mpenja wa kwa msaada wa Sportsmail
NYOTA Lewis Holtby ataruhusiwa kuihama klabu yake ya Tottenham kwa mkopo kama Christian Eriksen kutoka klabu ya Ajax atasajiliwa majira haya ya kiangazi.
Holtby, mwenye umri wa miaka 22, ameshindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Spurs tangu asajiliwe kutoka Schalke 04 ya Ujerumani mwezi januari mwaka jana.
Hana Jipya: Lewis Holtby ataruhusiwa kuondoka Tottenham kwa mkopo
Nyota huyo raia wa Ujerumani alicheza mechi 11 tu msimu uliopita, lakini bado ameendelea kukalia benchi baada ya kushindwa kucheza katika mechi tatu za ufunguzi za kocha Andre Villas-Boas.
Pia Spurs watasikiliza ofa kutoka ya Gylfi Sigurdsson kabla ya dirisha la usajili kufungwa jumatatu.
Wanaelekea kumnasa: Tottenham wameruhusiwa kuongea na Ajax juu ya usajili wa Christian Eriksen (kulia)
0 comments:
Post a Comment