Thursday, August 8, 2013


Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Klabu ya Roma inayocheza ligi kuu nchini Italia, Seria A,  imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa Arsenal yenye makazi yake kaskazini mwa London, Gervinho kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni saba.
Nyota huyo raia wa Ivory Coast alishindwa kuonesha makali yake tangu ajiunge na Arsenal mnamo mwaka 2011 na sasa anatarajia kufanya kazi na kocha wa Roma, Rudi Garcia, ambaye ni kocha wake wa zamani akiwa klabu ya Lille ya Ufaransa,  na pengine ataonesha cheche zake  kama enzi zake akiwa klabu ya  Lille ya Ufaransa.
Mshambuliaji huyo ndio wa mwisho kuondoka katika klabu ya Asernal muda huu wakati kocha Arsene Wenger akisuka kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu soka nchini England na ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Happy ending: Gervinho's miserable spell at Arsenal has come to an endFuraha ya mwisho: Msimu mgumu kwa Gervinho katika klabu ya  Arsenal umefika tamati baada ya kukamilisha uhamisho kuelekea Roma.
Mapema katika majira haya ya kiangazi, mchezaji mwenye rekodi ya kusajiliwa kwa dau kubwa na Arsenal,  Andrey Arshavin alitimka zake baada ya mkataba wake kumalizika na wakati huo huo wachezaji Denilson,  Sebastien Squillaci, na Marouane Chamakh wanatarajia kufuata nyuma yake kutimka Emirates majira haya ya joto.
‘Nimefurahia kumsajili Gervinho kama nilivyofurahi baada ya kuwapata  Morgan De Sanctis na   Kevin Strootman, Alisema kocha wa Roma, Garcia.
‘Gervinho ni mchezaji wa haraka na kasi, anaweza kushambulia na ni mchezaji mwenye aina ya pekee ya mpira ukilinganisha na wachezaji wengine.’
GervinhoKaenda zake Serie A : Gervinho anatarajia kufanya kazi na  Rudi Garcia, kocha wake wa zamani akiwa  Lille
Talented: But Gervinho rarely showed his quality at The Emirates
Ana kipaji kikubwa:  Lakini Gervinho hajapata nafasi ya kuonesha ubora wake katika dimba la Emirates

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video