Mahmoud Ahmad, Arusha
Chama cha kuweka na kukopa cha Fahari yetu SACCOS kimeweza kuongeza idadi ya wanachama kwa asililmia 13%katika mwaka wa fedha 2011-12 na kupata faida ya tsh 69 milion kutokana vyanzo vya mapato ikiwemo riba ya mikopo,ada ya mikopo,ada ya kuchukuwa akiba na mauzo ya mpesa.
Hayo yamebainishwa na mweyekiti wa chama hicho kinachoundwa na wafanyakazi wa Taasisi ya mikopo ya PRIDE Tanzania Elias Ntambi wakati wa kufungua mkutano huo uliofuguliwa na Mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC jijini hapa.
Elias alisema kuwa mafanikio makubwa waliyopata katika chama chao yametokana na mazingira mazuri yaliowekwa na serekali yetkatika kuendeleza sekta hi pamoja na ushirikiano mzuri tunaopata kutoka katika idara ya ushirika jiji la Arusha hivyo kufanikiwa kuongeza wigo wa mafanikio.
Akabainisha kuwa miongoni mwa mafaniko waliopata kwa mwaka wa huu na uliopita ni kuongeza idadi ya wanachama kutoka 453 hadi511 sawa na aslimia 13% huku wakiongeza faida pia ya fedha kiasi cha tsh69,881,533 iliyotokana na vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwa ni pamoja na riba ya mikopo,ada ya mikopo,ada ya kuchukuwa akiba na mauzo ya m-pesa kutokana na faida hiyo wanatarajiwa kupata gawio la tsh.34,896,667 baada ya kutoa matengo ya akiba ya kisheria hii ni ongezeko la aslimia 18%.
Aidha Elias alisema kuwa akiba za wanachama hadi kufikia mwishoni mwa mwaka201 zimefikiwa tsh796,976,195 sawa na ongezeko la asilimia38.2% kulingana na akiba iliyowekwa mwaka huohuku mikopo iliyopo mikononi mwa wanachama ikifikia tsh1,283,306,417.
Elias alisema mkutono huo utakuwa ni wa siku moja pamoja na mengine utajadili na kupokea taarifa za mahesabu ya mwaka uliopita2012 na kujadili taarifa ya utendaji wa chama hicho na kupitisha bajeti ya mwaka 2013-14 aidha utafanya uchaguzi wa kujaza nafasi za wajumbe wa bodi na kamati ya usimamizi kwa mujibu wa katiba yetu na sheria ya vyama vya ushirika.
Akizungumza wakati akifungua mkutano huo DC kasunga alisema kuwa ndani ya mkutano huo wanachama watapata fursa nzuri kuhoji na kuomba kueleweshwa kuhusu mauasla mbambali yanayohusu mustakabali wa chama chenu hivyo ni fursa nzuri kutumia kwa mustakabali wa chama chenu.
Alisema kuwa kwa kuwa mkutano huu mkuu wa chama chenu ndicho chmbo chenye maamuzi ya juu mkitumie kuweka malenge ya kuongeza wigo wa kupata wanachama wapya ilikuweza kuwa na chama chenye nguvu kitakachosaidia ukuaji wa uchumi wa wanachama na taifa kwa ujumla wake.
“Hapa sintakuwa mchoyo wa kuwapa pongezi kwa mafanikio mliopata kwa mwaka uliopita nikitarajia mafanikio haya kuwa changamoto kwenu ya kufanya vizuri zaidi ya hapa katika kipindi kijacho”alisema Kasunga.
Kasunga Aliwataka kufahamu vyema wajibu na majukumu yao kama wanachama kwa kutimiza wajibu wao wa kuweka akiba mara kwa mara,kukopa kwa busara na kurejesha mikopo kwa wakati ni dhahiri kwamba chama kitakuwa katika mwelekeo mzuri wa kutimiza azma yake ya kuboresha maisha na kuwapa huduma bora zenye masharti nafuu wanachama wake.
Akabainisha mkakati wa serekali yetu wa matokeo makubwa sasa(BIG RESULT NOW)hautafanikiwa kuharakisha maendeleo ya nchi yetu endapo watu binafsi pamoja na sekta zote za serekali na umma hazitafanyakazi zake kwa ufanisi wa hali ya juu na huvyo ninyi ni kama sehemu ya jamii tunategemea sana mchango wenu katika kufanuikisha mkakati huu na kujilete maendeleo na maisha bora.
0 comments:
Post a Comment