Saturday, August 10, 2013


100_1462
Na Braka Mpenja 
Kocha mpya wa klabu ya Njombe Mji ya mkoani Njombe, ambaye ni mjumbe wa kamati ya ufundi ya Simba, John Wiliam “Del Piero” amefurahishwa na kuendelea kwa ligi ya mabingwa wa wilaya mkoani humo na ameshaanza kupita katika mechi hizo ili kuona wachezaji wa kuwasajili.
Akizungumza na Mtandao wa MATUKIO DUNIANI kwa njia ya simu leo hii, Piero amesema katika mechi chache alizopita ameona vipaji vya hali ya juu, lakini vinahitaji kuendelezwa zaidi.
“Kuna vipaji vingi ujue, kuna vijana wanacheza mpira mzuri japokuwa kuna waalimu wachache wa kuwaendeleza, lakini tutaendelea vizuri zaidi na kupata wachezaji wakali”. Alisema Piero.
Piero ambaye alikuwa kocha wa Mabingwa wa zamani wa soka Tanzania, Africans Sports ya Tanga aliongeza kuwa viongozi wa Njombe Mji wamejipanga na wanampa ushirikiano mkubwa sana, hivyo anaamini watakuwa na timu nzuri zaidi.
“Viongozi wangu wako vizuri, kila mtu anatekeleza majukumu yake, mimi nikiwa mwalimu nina kazi zangu za kitaaluma, lakini wako bega kwa bega na mimi kuhakikisha wananisaidia kupata wachezaji wazuri”. Alisema Piero.
Hata hivyo kocha huyo ambaye  alisema kuwepo kwa kocha Nsajigwa katika klabu ya Lipuli inayoshirki ligi daraja la kwanza kutamfanya apate mechi za majaribio kutoka kwake kwani timu yake ni kubwa na watajifunza mambo mengi kutoka kwake.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video