Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mabingwa wa ligi kuu soka nchini England, klabu ya Manchester United inaendelea kumfuatilia mshambuliaji hatari wa klabu ya Real Madrid ya Hispania na timu ya Taifaya Ureno Cristiano Dos Santos Aveiro Ronaldo baada ya makocha Phil Neville na Steve Round kumshuhudia nyota huyo wa zamani wa Old Trafford akiichezea Ureno jana usiku.
Neville na Round walikuwa kwenye Uwanja wa Algarve kumshuhudia Ronaldo akifunga bao dakika za lala salama na kuinusuru Ureno kuzama mbele ya Uholanzi kwa kupata sare ya 1-1 ya Robin Van Persie.
United imetunza jezi namba saba (7)zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya kuanza kwa msimu mpya kwa matumaini ya kutimiza ndoto za kumrejesha Ronaldo kutoka Real Madrid – miaka minne baada ya kutimkia Bernabeu kwa sau la rekodi ya dunia, Pauni Milioni 80.


Hatima ya nyota huyo umeendelea kuwa ya mashaka nchini Hispania, licha ya Rais wa Real, Florentino Perez kuhakikisha kwamba atasaini Mkataba mpya.
David Moyes na Mtendaji Mkurugenzi mpya wa United, Ed Woodward wakiwa bado hawajasajili mchezaji yeyote tangu waanze kazi na tetesi zikizidi juu ya Wayne Rooney kuondoka.
Manchester United inafahamu kwamba kumnasa Ronaldo watawapa presha kubwa wapinzani wao wote ndani na nje ya uwanja
Enlarge
Vipi mwanangu? Ronaldo akipeana hai na Arjen Robben kabla ya kuanza kwa mechi hiyo jana usiku


Usafi nao muhimu jamani: Ronaldo akitengeneza nywele zake kabla ya kuanza kwa mechi ya jana
0 comments:
Post a Comment