Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Ripoti kutoka nchini Hispania zinaeleza kuwa beki wa kati wa Chelsea, David Luiz amevunja ukimya na kumuambia meneja wake Jose Mourinho kuwa anataka kuihama klabu yake na kujiunga na Fc Barcelona.
Beki huyo raia wa Hispania ni miongoni mwa wachezaji wanaowindwa na kocha wa Barca, Gerardo Martino majira haya ya kiangazi na lengo lake likiwa ni kupata mlinzi mzuri wa kati kuimarisha ukuta wake uliogeuka kuwa uchochoro msimu uliopita.
Luiz ameichezea Chelsea kwa miaka miwili na nusu akisajiliwa kwa ada ya pauni milioni 25 kutoka Benfica na kuonesha kiwango cha juu na kuwa miongoni mwa mabeki wa bora ligi kuu nchini England.
Raha kwa Barca: David Luiz amewaambia Chelsea kuwa anataka kutimkia Barcelona
Taarifa hizi ni kwa mujibu wa gazeti la Mundo Deportivo
Luiz amekuwa katika harakati za kujiunga na Barcelona baada ya dili la Thiago Silva, aliyekuwa akitajwa kujiunga Camp Nou kubuma
Kocha Jose Mourinho hakufurahishwa na kiwango cha Luiz mechi za nyuma, lakini alisema nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 hatauzwa majira haya ya kiangazi.
Gazeti ka Hispania la Mundo Deportivo jana lilieleza kuwa Barcelona wameshatuma ofa ya kwanza ya pauni milioni 25 ambayo Chelsea walicheka sana, ingawa pesa hiyo inayoonekana ndogo imekubaliwa na mchezaji na kuonesha nia ya kusepa zake darajani.
Msimamo wa Luiz umewapa moyo Barca, na sasa wanajiandaa kupandisha dau hadi kufikia pauni milioni 31, japokuwa itakuwa imepungua pauni milioni 12 kwa kiasi ambacho Chelsea wanahitaji.
Beki wa Barca ambaye anatoka na Luiz nchini Brazil, Dani Alves amepiga kampeni kubwa ili asajiliwe na Barca, lakini amekiri kuwa kocha Jose Mourinho hawezi kumuachia kirahisi Mbrazil mwenzake.
Mtu bosi: Kocha mpya wa Barcelona, Gerardo Martino amejiingiza katika harakati za kuitaka saini ya Luiz majira haya ya kiangazi
0 comments:
Post a Comment