Na Baraka Mpenja
Wakati najaribu kupita katika kurasa za wachezaji wa kibongo na wa Mbele kuangalia wameandika nini katika akaunti zao za mitandao ya kijamii ikewo facebook na Twitta, kwa lengo la kupata mawazo yao kuhusiana na mambo mengi ya maisha yao na soka nimekutana na kioja cha mchezaji mmoja wa hapa nyumbani Tanzania.
Homa ya pambano la ngao ya jamii baina ya Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara, klabu ya Yanga dhidi ya Makamu Bingwa, Azam Fc ukitarajia kupigwa kesho kutwa uwanja wa Taifa ikizidi kupanda, hii leo Beki wa kati wa klabu ya Yanga, Nadir Haroub “Canavaro” katika Ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook ameandika maneno yafuatayo:
“Huu ndiyo msimu ambao tumepanga kuwapiga 8-0 wale watoto wa shule ….nadhani mnawajua…. samahani lakini..”
Binafsi nimetafakari kauli yake akimaanisha nini, najua na kila mtu anajua kuwa wapinzani wakubwa wa Canavaro ni Simba, na msimu wa mwaka juzi Simba waliwafunga Yanga mabao 5-0 na msimu uliopita Yanga walishinda mabao 2-0 mchezo wa kufungia pazia la ligi kuu.
Je, anamaanisha hizo goli 8 watawafunga akina nani msimu unaotarajia kuanza Agosti 24 mwaka huu?, Ni Simba au Azam fc au klabu ipi?
Kesho nitamuuliza Canavaro, fuatilia mtandao huu….
0 comments:
Post a Comment