Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
MABINGWA wa Bundesliga na UEFA , Wekundu wa kusini mwa Ujerumani, Bayern Munich wamebeba ubingwa wa Super Cup baada ya kuifunga Chelsea kwa mikwaju 5-4 ya penati.
Katika muda wa kawaida timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2 baada ya Chelsea kuanza kufunga katika dakika ya nane tu kupitia Fernando Torres.
Mechi hiyo ilikwenda hadi dakika 120 kabla ya kusogezwa kwenye mikwaju ya penalti. Kama Lukaku angefunga mkwaju wa mwisho, Chelsea ingekuwa bingwa, lakini akapiga na kipa Neuer akapangua.
Kikosi cha Bayern Munich: Neuer, Rafinha (Javi Martinez 56), Dante, Boateng, Alaba, Muller (Gotze 70), Lahm, Kroos, Ribery, Mandzukic, Robben (Shaqiri 95).
Wachezaji wa akiba: Starke, Van Buyten, Contento, Pizarro.
Waliopata kadi: Ribery
Mabao: Ribery (47), Javi Martinez (120)
Kikosi cha Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Luiz, Cole, Ramires, Lampard, Hazard, Oscar, Schurrle, Torres (Lukaku 97).
Wachezaji wa akiba: Schwarzer, Azpilicueta, Terry, Essien, Mikel, Mata.
Waliooneshwa kadi: Cahill, Ramires, Luiz, Torres, Cole, Ivanovic
Kadi nyekundu: Ramires (84)
Mabao: Torres (8) Hazard (93).
Lukaku haamini baada ya kukosa penati
Mabingwa tena: Bayern wakishangilia baada ya kipa wao Neuer kuokoa mkwaju wa penati
Akihabaribu mambo: Javi Martinez (kulia) aliisawazishia Bayern dakika za mwisho za nyongeza
0 comments:
Post a Comment