Mabingwa wa soka Tanzania bara, klabu ya Yanga ya Dar es salaam leo wameonesha umwamba wao baada ya kuwazamisha wakata miwa wa Manungu Turiani mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar, mabao 3-1 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Katika mchezo wa leo, Yanga walikuwa wa kwanza kuandika bao katika dakika ya 26 kupitia kwa mshambuliaji wake anayerejesha makali yake, Said Bahanuz. Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Mtibwa Sugar walisawazisha bao hilo katika dakika ya 57 kwa njia ya mkwaju wa penati iliyopigwa na mtaalamu Shaban Kisiga “Malone” baada ya beki aliyesajiliwa kutoka Mtibwa, Rajab Zahir kuunawa mpira eneo la hatari.
Katika dakika ya 81 mshambuliaji wa Yanga, Jerryson Tegete aliandika bao la pili kwa njia ya penati baada ya yeye mwenyewe kuangushwa eneo la maguu 18 ya mtu mzima na beki Salvator Ntebe akielekea kutia mpira kambani.
Mshambuliaji wa wanajangwani aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar, Hussein Javu hakuwa na huruma hata kidogo baada ya kuifungia Yanga bao la tatu dakika ya 87 na kuhitimisha shangwe, nderemo na vifijo kwa kwalalumpa Malysia.
Hata hivyo kipnidi cha kwanza, Mtibwa Sugar walipata nafasi za kufunga, lakini walishindwa kuzibadili kuwa magoli.
Baada ya mechi hiyo, Kocha wa Mtinwa Sugar, Mecky Mexime amesema mechi ya leo ilikuwa nzuri kwa timu zote mbili na ameitumia vizuri kubaini makosa ya kikosi chake.
“Mechi ilikuwa nzuri yenye changamoto kubwa, kikosi changu kimecheza vizuri na kupata nafasi za kufunga, lakini kukosa umakini kumewagharimu, ila narudi kuwanoa tena kabla ya kuanza kwa ligi kuu soka Tanzania bara”. Alisema Mexime.
Kikosi cha Dar Yonug Africans kilikuwa: Deo Munishi ‘Dida’/Ally Mustafa ‘Barthez’ dk46, Juma Abdul, Oscar Joshua/David Luhende dk46, Issa Ngao, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Athumani Iddi ‘Chuji’/Rajab Zahir dk46, Said Bahanuzi/Abdallah Mnguli ‘Messi’ dk 71, Salum Telela, Shaaban Kondo/Hussein Javu dk46, Jerry Tegete na Haruna Niyonzima.
Wana Tamtam Mtibwa Sugar; Hussein Sharif ‘Cassilas’/Said Mohamed dk53, Hassan Ramadhani, Paul Ngalema, Ally Lundenga/Dickson Daudi dk64, Salvatory Ntebe, Salum Mbonde, Ally Shomari, Masoud Ally, Abadallah Juma, Shaaban Kisiga ‘Malone’ na Ally Mohamed
0 comments:
Post a Comment