Sunday, August 11, 2013

yanga1
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara , klabu ya Yanga ya Dar es salaam, leo hii wanajitupa  katika dimba la Taifa, jijini Dar es salaam  kuvaana na Sports Club Villa ya Uganda katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
Yanga wanaingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kushinda mechi mbili zilizopita za kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo walishinda mabao 3-1 na mchezo mwingine walishinda bao 1-0 dhidi ya 3Pillars ya Nigeria.
Villa wanaingia uwanjani ikiwi ni saa chache zimepita tangu wapokee kipondo kikali cha mabao 4-1 kutoka kwa Wekundu wa Msimbazi Simba katika mchezo wa kirafiki uliofanyika jana uwanja wa Taifa ukiwa ni maalumu kusindikiza tamasha la Simba Day.
Mechin hiyo kali iliyopigwa mbele ya wanachama, mashabiki na viongozi wa Simba na wa timu pinzani ilikuwa kali ya kusisimua huku Kikosi cha Simba kikicheza soka safi, lakini mpaka dakika dakika 45 zikimalika, miamba hiyo ya soka la Afrika mashariki na kati ilikuwa imechoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1, huku waganda wakiwa wa kwanza kufunga bao lao.
Simba walisawazisha mufa mfupi kabla ya kwenda mapumziko kupitia kwa nyota wake kinda Gerrard Jonas Mkude na kuibua shangwe na nderemo kubwa kwa mashabiki wa Simba.
 Kipindi cha pili Simba walianza kwa kasi na kuonesha soka safi la kufundishika huku mashabiki wake wakishangilia kwa nguvu zote kutokana  utaalamu mwingi wa kikosi chao kinachonolewa na kocha mzalendo, Abdallah King Kibaden Mputa.
Wekundu wa Msimbazi waliongeza bao la pili katika dakika ya 9 kipindi cha pili, kupitia kwa kinda lao, Wiliam Lucian aliyepiga shuti kali na kutinga nyavuni.
Katika dakika ya 25 kipindi cha pili, Betram Mombeki aliandika bao la tatu na kuzidi kuwapa raha mashabiki wa Simba waliokuwa wanashangilia kwa staili ya kuwakejeli mashabiki wa upande wa pili walioonekana kuwa kimya muda mwingi.
Katika dakika ya 28, Mombeki aliandika bao la nne na kuonekana kama dawa halisi ya kufunga mabao kwa wekundu wa Msimbazi Simba kwa lugha ya mtaani “Mtambo wa magoli”.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video