Tuesday, July 9, 2013

YErnie-Brandts
Kocha mzungu wa mabingwa wa soka Tanzania bara, Dar Young Africans, Mholanzi Ernie Brandts (Juu) atapimana maarifa ya soka na kocha mzawa wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime (Chini)  katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika Alhamisi ya Julai 11 katika Dimba la Ally Hassani Mwinyi mjini Tabora. Msimu uliopita, Brandts alimvulia kofia Mexime, acha tusubiri hiii mechi yao ya kujipima ubavuSONY DSC
Na Baraka Mpenja 
Mabingwa wa soka Tanzania bara kwa msimu wa 2012/2013, klabu ya Yanga ya Dar es salaam, “Kwalalumpa Malysia” wamemaliza ziara yao mikoa ya kanda ya ziwa na leo hii asubuhi wanatarajiwa kuondoka mkoani Shinyanga kuelekea kwa wanyamwezi, mkoani Tabora kucheza mchezo wao mwisho wa kirafiki dhidi ya wakata miwa wa mashamba ya miwa ya Manungu Turiani mji kasoro bahari, Morogoro, klabu ya Mtibwa Sugar, katika uwanja uwanja wa Ally Hassan Mwinyi.
Afisa habari wa Yanga waliozoeleka kuvaa uzi wa njano na kijan, wenya makazi yao mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es salaam, Baraka Kizuguto, ameimbia MATUKIO DUNIANI kuwa wachezaji wote wapo salama baada ya mitanange miwili ya jijini Mwanza na Shinyanga dhidi ya mabingwa wa Uganda, klabu ya KCC.
“Timu imefanya mazoezi jana, wachezaji wote wapo salama, tunaondoka leo asubuhi kuelekea mkoani Tabora ambapo tutacheza na wakata miwa wa Manungu ikiwa ni muendelezo wa michezo ya kirafiki kunoa makali yetu kabla hatujaanza kazi ya kutetea ubingwa wetu tuliotwaa msimu uliopita”. Alisema Kizuguto.
Yanga walionza ziara yao jijini Mwanza kwa lengo la kuwaonyesha kombe mashabiki wao, walipokelewa kwa shangwe na nderemo kubwa na mashabiki wao, lakini katika mechi yao ya kwanza dhidi ya KCC katika dimba la CCM Kirumba waliambulia suluhu pacha ya bila kufungana, na katika mchezo wa marudiano uwanja wa Kambarage Mkoani Shinyanga waliambulia kipigo cha 2-1.
Kizuguto alisema licha ya kushindwa kufanya vizuri, bado watu wa kanda ya ziwa wameonekana kuwaunga mkono zaidi na kujitokeza kwa wingi katika mazoezi na mechi za huko.
“Yanga muziki wake ni mkubwa, watu wanafurika vibaya sana, kikubwa tunawaomba mashabiki na wanachama wetu kuendelea kutuunga mkono zaidi kwani ndio kwanza tumeanza maandalizi”. Alisema Kizuguto.
Pia afisa habari huyo alisema makocha wa klabu hiyo, Mzungu kutoka Uholanzi, Ernie Brandts na Mtanzania Fred Ferlix Minziro wameona nini cha kufanya katika kikosi chao hivyo timu ikirejea jijini Dar es salaam wataongeza kuwanoa zaidi wanandinga wao.
“Mipango yetu ni kutetea ubingwa wa ligi kuu na kufanya vizuri michuano ya kimataifa, hivyo jitihada kubwa zinafanywa na makocha wetu kuhakikisha maandalizi yanakuwa mazuri na kikosi kinajengeka”. Alisisitiza Kizuguto.
Kizuguto alisema wanajiandaa na mchezo wa julai 13 dhidi ya Mtibwa Sugar na julai 12 watarejea jijini Dar es salaam.
“Baada ya mechi ya Mtibwa tutarejea Dar kuendelea na mipango mingine ya mazoezi, kikubwa ni kuombeana dua njema ili tusafiri salama”. Alisema Kizuguto.
Wakati Yanga wakisafiri leo kuelekea Tabora, kwa upande wa Mtibwa Sugar wamesema wanaendelea na mazoezi yao na siku ya jumatano (Julai 10) watasafiri kuelekea mkoani humo.
Kocha wa klabu hiyo, nahodha wa zamani wa Taifa Stars mwenye historia ya kuzikataa Simba na Yanga enzi za maisha yake ya soka, Mecky Mexime alisema vijana wote wapo salama na anajiandaa kuwakabili Yanga, ingawa mchezo huo wa kirafiki ni mazoezi kwao na maandalizi ya ligi kuu, hivyo hajachukulia uzito mkubwa sana.
“Ujue ndio tunajiandaa na msimu mpya, ni mechi ya maandalizi tu, haina ishu sana, lakini tulifanya mazoezi jana jioni, na leo tunatarajia kujifua na hapo kesho tunaondoka zetu kwenda Tabora”. Alisema Mexime.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video