Mbunge
wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (mwenye Suti) na
katibu wa Chadema Iringa mjini Suzana Mgonakulima wa kwanza kushoto
wakiwa na madiwani wa CCM katika msiba wa diwani Chonanga leo
Msaidizi
wa askofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT)
dayosisi ya Iringa Blaston Gavile akiendesha ibada ya mazishi ya
diwani Chonanga leo makaburi ya Mtwivila mjini Iringa
Hili
ni gari ambalo lilkuwa likiufuata msafara wa waziri mkuu jambo
ambalo lingeweza kusababisha ajali katika msafara huo hapa ni eneo la
Mtwivila mjini Iringa
Mlezi
wa CCM mkoa wa Iringa waziri mkuu Mizengo Pinda (kushoto ) mkewe Tunu
Pinda wakiweka shada la maua katika kaburi la diwani Iddi Chonanga
leo
Waziri mkuu Pinda akimsubiri mke wake Tunu Pinda aweke shada ya maua kabla ya kutoa heshima yao ya mwisho leo
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma akiweka shada la maua katika kaburi ya diwani Chonanga leo
Mbunge
wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) na mbunge wa
viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) wakishirikiana kuweka
shada la maua katika kaburi la diwani Iddi Chonanga ,enzi za uhai
wake diwani Chonanga na familia yake walikuwa wakikabiliwa na kesi
ya kumtishia kumuua mbunge Msigwa kwa maneno kesi ambayo bado hukumu
yake kutolewa
Mbunge
wa jimbo la Kilolo na MNEC Prof Peter Msolla na mbunge wa viti maalum
mkoa wa Iringa Lediana Mafulu wakiweka shada la maua katika kaburi la
Chonanga leo
Mstahiki
meya wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi akipokea shada kutoka kwa
afisa habari Manispaa ya Iringa Sima Bingileki ili kuweka katika
kaburi la diwani Chonanga
Naibu
meya wa Manispaa ya Iringa Bw Gervas Ndaki kushoto akiongoza
madiwani kuweka mashada ya maua katika kaburi la diwani Chonanga leo
Katibu
wa Chadema Iringa mjini na diwani wa viti maalum Suzana Mgonakulima
kushoto akiweka shada la maua katika kaburi la Diwani mwenzake
Chonanga
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Terresia Mahongo akiweka shada la
maua leo kwenye kaburi la diwani Iddi Chonanga
Picha na habari na Francis Godwin Blog- Mzee wa matukio Daima
WAZIRI
mkuu Mizengo Pinda ambae ni mlezi wa chama cha mapinduzi (CCM)
mkoa wa Iringa leo ameongoza wakazi wa mkoa wa Iringa katika
mazishi ya aliyekuwa diwani wa kata ya Nduli marehemu Iddi Rashid
Chonanga huku akijitolewa kusomesha watoto wake wawili na yatima
mmoja aliyekuwa akisomeshwa na marehemu Chonanga.
Waziri Pinda alitoa ahadi
leo katika makaburi ya Mtwivila mjini Iringa wakati akitoa salam
zake za rambi rambi kwa wakazi wa kata ya Nduli na wananchi wa mkoa
wa Iringa kufuatia kifo cha diwani huyo .
Alisema
kuwa kifo cha diwani Chonanga kimeacha pendo ndani ya familia na
hata katika chama chake cha CCM kutokana na mchango mkubwa ambao
amepata kuutoa katika kupigania chama hicho na kuwa kutokana na maombi
kusomeshwa yaliyotolewa na watoto hao ambao waliyatoa jana
alipofika kuhani msiba huo katika kijiji cha Nduli
Kuwa kwa upande wake amejitolea kuisaidia familia hiyo
ya Chonanga kwa kusomesha mtoto mmoja anayeendelea na masomo katika chuo cha IFM jijini Dar es Salaam pia kumsomesha kijana wake mmoja ambae yupo sekondari pamoja na kuendelea kumsomesha mtoto mmoja yatima ambae diwani Chonanga alikuwa akimsomesha katika shule ya Sekondari ya Miyomboni mjini Iringa.
ya Chonanga kwa kusomesha mtoto mmoja anayeendelea na masomo katika chuo cha IFM jijini Dar es Salaam pia kumsomesha kijana wake mmoja ambae yupo sekondari pamoja na kuendelea kumsomesha mtoto mmoja yatima ambae diwani Chonanga alikuwa akimsomesha katika shule ya Sekondari ya Miyomboni mjini Iringa.
Mbali
ya kujitolea kusomesha watoto hao bado waziri Pinda alilitaka
baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na mkurugenzi
wa Halmashauri hiyo kuangalia uwezekano wa kumuenzi diwani Chonanga
kwa kazi kubwa za maendeleo alizozifanya katika kata yake kwa
kuisaidia
familia yake .
familia yake .
“
Mimi nawashauri madiwani pamoja na mkurugenzi wa Manispaa kutokana na
mchango mkubwa ambao diwani Chonanga aliutoa katika kuwatumikia
wananchi wa kata ya Nduli ….sasa kuangalia uwezekano wa kuisaidia
familia yake…..sisi kama chama leo tulikuwa na Halmashauri kuu ya CCM
tumechangishana kiasi cha zaidi ya Tsh 800,000 ambazo tunazikabidhi
kwa familia”
Katika
hatua nyingine waziri Pinda amekipongeza chama cha Demokrasia na
maendeleo (Chadema) wilaya ya Iringa mjini chini ya mbunge wa jimbo
la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa
katika mazishi hayo .
“
Kweli kwa moyo mkunjufu kabisa napenda kuwashukuru sana viongozi
wa Chadema Iringa chini ya mbunge mchungaji Msigwa kwa ushiriki mzuri
wa mazishi ya diwani Chonanga ….nasema ahsanteni sana mheshimu mbunge
Msigwa na wananchi wote ambao leo mmefika hapa”
Awali
akiendesha ibada ya mazishi hayo msaidizi wa askofu wa kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa Blaston Tuluwene Gavile alitaka
viongozi wa serikali na kisiasa kukumbuka kumcha Mungu na kuiga
mfano wa Chonanga ambae mbali ya kufanya shughuli za kisiasa ila
katika dini alikuwa mstari wa mbele akiwa kama mshauri wa usharika wa
Nduli .
Nduli .
Alisema kuwa mara kwa mara Chonanga alikuwa akipigania maendeleo ya
kata yake ya Nduli na wananchi wake na kuna wakati alipata kumtamkia wazi wazi kuwa yupo tayari kufa na hata agopa binadamu yeyote katika kuwapigania wananchi wake.
kata yake ya Nduli na wananchi wake na kuna wakati alipata kumtamkia wazi wazi kuwa yupo tayari kufa na hata agopa binadamu yeyote katika kuwapigania wananchi wake.
“ Marehemu alikuwa mtetezi wa kweli wa maendeleo ya wananchi wake
ndani ya chama chake na hata katika kanisa pia ndio maana leo umati mkubwa wa watu wamejitokeza kumzika ila sisi kama kanisa tunasema kifo katika Kristo ni furaha kubwa na leo hii mama mzazi wa Chonanga ambae ana miaka zaidi ya 83 ameomba kubatizwa rasmi “
ndani ya chama chake na hata katika kanisa pia ndio maana leo umati mkubwa wa watu wamejitokeza kumzika ila sisi kama kanisa tunasema kifo katika Kristo ni furaha kubwa na leo hii mama mzazi wa Chonanga ambae ana miaka zaidi ya 83 ameomba kubatizwa rasmi “
Akisoma
histori ya marehemu Chonanga mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Iringa Terresia Mahongo alisema kuwa Chonanga alizaliwa mwezi
Februari ,1947 katika kijiji cha Malolo wilaya ya Kilosa na elimu
yake ya msingi aliipata katika shule ya kati ( Middle School ) Kidodi
wilaya ya Kilolo na kujiunga na mafunzo ya ualimu katika chuo cha
ualimu Songea mkoani
Ruvuma mwaka 1970
Ruvuma mwaka 1970
Katika
uhai wake marehemu aliajiriwa kama mwalimu wa shule ya msingi mwaka
1972 ambapo miongoni mwa shule alizopata kufundisha ni pamoja na
Mwembetogwa ,Kilimani , Nyabula, Nduli na Kitelewasi zilizopo mkoani
Iringa pia marehemu aliwahi kuwa mratibu elimu kata ya kalenga kuanzia
mwaka 1994-1999 alipostaafu kwa mujibu wa sheria na mwaka 2000
alifanya kazi ya ualimu kwa mkataba wa mwaka mmoja
Katika
uongozi amepata kuwa mwenyekiti wa CCM kata ya Nduli kati ya mwaka
2000-2005 na mwaka 2010 alichaguliwa kuwa diwani wa kata ya Nduli
katika Halmashauri hiyo ya Manispaa ya Iringa na katika baraza la
madiwani
wa Halmashauri hiyo alikuwa ni mwenyekiti wa kamati ya maadili na mjumbe wa kamati ya fedha na uongozi .
wa Halmashauri hiyo alikuwa ni mwenyekiti wa kamati ya maadili na mjumbe wa kamati ya fedha na uongozi .
Mkurugenzi huyo alisema kuwa katika kipindi cha uongozi wake alikuwa ni
jasiri ,mfuatiliaji wa mambo,mshauri na mjenga hoja katika vikao vya madiwai .
jasiri ,mfuatiliaji wa mambo,mshauri na mjenga hoja katika vikao vya madiwai .
Marehemu Chonanga alianza kusumbuliwa na maradhi
ya moyo usiku wa tarehe 2/7/2013 na alfajiri ya tarehe 3/7/2013
alipelekwa Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kupata matibabu na mbali ya jitihada zilizofanywa na madaktari ila zilishindikana na majira ya saa 7;45 mchana alifariki dunia .marehemu Chonanga ameacha mjane mmoja watoto 10 na wajukuu 9
Mungu ailaze roho ya marehemu Iddi Rashidya moyo usiku wa tarehe 2/7/2013 na alfajiri ya tarehe 3/7/2013
alipelekwa Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kupata matibabu na mbali ya jitihada zilizofanywa na madaktari ila zilishindikana na majira ya saa 7;45 mchana alifariki dunia .marehemu Chonanga ameacha mjane mmoja watoto 10 na wajukuu 9
Chonanga mahali pema peponi Amina
0 comments:
Post a Comment