Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu wa pili kulia akitoa
akiitambulisha familia ya marehemu diwani Idd Chonanga aliyekuwa
diwani wa kata ya Nduli aliyefariki dunia jana
Mtoto
mkubwa wa marehemu Idd Chonanga Bw Greyson Chonanga akipewa mkono
wa pore na waziri mkuu Mizengo Pinda aliyefika nyumbani kwao eneo la
kijiji cha Nduli kuhani msiba huo jioni ya leo ,anayeshuhudia ni
mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu
Viongozi
mbali mbali wa CCM na serikali mkoa wa Iringa wakiwa na waziri mkuu
Mizengo Pinda pamoja na waombolezaji wa msiba wa aliyekuwa diwani wa
kata ya Nduli Idd Chonanga aliyefariki jana
Waziri
Pinda akiwapa pole wafiwa leo katika msiba wa diwani wa kata ya Nduli
mjini Iringa Idd Chonanga aliyefariki dunia jana
Msafara
wa waziri mkuu Mizengo Pinda ukitoka kuhani msiba wa diwani wa kata
ya Nduli Idd Chonanga aliyefariki jana na kuzikwa kesho kijijini hapo
|
kada wa CCM mzee My Studio akisalimia na waziri mkuu |
Jembe la manispaa ya Iringa mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa Teresia Mahongo akimpokea waziri mkuu Mizengo Pinda kwa tabasamu kali |
Makada wa CCM familia ya My Studio |
Wadau wa masuala ya utalii mkoa wa Iringa ambao wanapigania kuitangaza hifadhi ya Ruaha na hifadhi za kusini |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo JOseph Muhumba akisalimiana na waziri Pinda |
Kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Abri Asas akiteta jambo na waziri mkuu Mizengo Pinda katika uwanja wa Ndege Nduli leo |
…………………………………………………………………
WAZIRI
mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Pinda ambae ni mlezi
wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa jioni ya leo amewasili
mkoani Iringa na kufika nyumbani kwa aliyekuwa diwani wa kata ya
marehemu Idd Chonanga na kuungana na waombolezaji katika kuifariji
familia ya diwani huyo.
Waziri
Pinda ambae aliongoza na mkewe mama Tunu Pinda na viongozi wengine wa
CCM mkoa wa Iringa pamoja na viongozi wa serikali ya mkoa wa
Iringa wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma
walifika nyumbani kwa marehe mu Chonanga eneo la Nduli majira ya saa
10.56 na kutumia muda wa zaidi ya dakika 10 kuifariji familia hiyo.
Akiwa
nyumbani kwa marehemu Chonanga waziri Pinda na mkewe wametoa pore
kwa familia hiyo ya Chonanga na kuwaomba kuendelea kuwa na
uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo na kuwa wao
katika chama wapo pamoja na familia hiyo katika maombolezo hayo .
Waziri
Pinda amesema kuwa binafsi kama mlezi wa CCM mkoa wa Iringa
ameguswa na kifo cha diwani Chonanga na kuwa kutokana na kuwa katika
ziara ya kichama mkoa wa Iringa ameona ni vema kabla ya kuanza
shughuli za chama kufika kuhani msiba huo .
Kwa
upande wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu
alisema kuwa CCM wilaya ya Iringa mjini na mkoa kwa ujumla wamepata
pigo kubwa kwa kifo cha diwani huyo na kusema kuwa CCM itashiriki
kwa asilimia 100 mazishi hayo yatakayofanyika mapema kesho katika
kijiji hicho cha Nduli.
Kwa
upande wake Greyson Chonanga ambae ni mtoto wa marehemu Chonanga
ameeleza kufurahishwa na hatua ya waziri mkuu kufika kuhani msiba
huo na kuwa wao kama familia hawakutambua kuwa msafara mkubwa kama
huo wa kitaifa ungefika kuhani msiba huo.
Huku
wakazi wa eneo hilo la Nduli wameelezwa kufurahishwa na umoja wa
kweli uliopo ndani ya serikali ya CCM kutokana na viongozi wake
kuwajali watu wa chini wanaowaongoza na kuwa utu ambao waziri mkuu
ameonyesha ni upendo tosha kwa wana Nduli kwa serikali ya CCM.
Alisema
Adam Kalinga mkazi wa kata hiyo ya Nduli ambae alikuwepo msibani
hapo kuwa katika kuenzi kazi za marehemu Chonanga wao wataendelea
kutambua mchango wake .
Diwani
Chonanga alifikishwa katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa jana
majira ya saa 12 asubuhi na majira ya saa 8 mchana alifariki dunia
kutokana na kusumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa BP ya kushuka
HABARI NA PICHA ZOTE KWA HISANI YA FRANCIS GODWIN- IRINGA
0 comments:
Post a Comment