RAIS TENGA KUFUNGUA KOZI YA BEACH SOCCER
Na Boniface Wambura, TFF
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga atakuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kozi ya mpira wa miguu wa ufukweni (beach soccer) itakayoanza leo (Julai 9 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Kozi hiyo itafanyika kwa wiki nzima kwenye klabu ya Escape iliyoko karibu na Safari Carnival, Mikocheni karibu na makao makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)- JKT Mlalakuwa. Uzinduzi utafanyika saa 3 kamili asubuhi.
Washiriki wa kozi hiyo itakayokuwa chini ya wakufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ni 60 ambapo 30 ni makocha wa mpira wa miguu na 30 wengine ni waamuzi wa mpira wa miguu.
Wakufunzi hao wa FIFA ni Angelo Schirinzi kutoka Uswisi kwa upande wa makocha wakati George Postmar kutoka Uholanzi ndiye atakayewanoa waamuzi.
PROGRAMU YA MAZOEZI YA TAIFA STARS
Taifa Stars chini ya Kocha Kim Poulsen inaendelea kujinoa jijini Dar es Salaam tayari kuikabili Uganda (The Cranes) katika mechi ya kufuzu kwa Fainali za Afrika kwa Wazhezaji wa Ligi za Nyumbani (CHAN) itakayochezwa Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ratiba ya mazoezi kwa Taifa Stars ni kama ifuatavyo;
Jumanne- Julai 9 mwaka huu Saa 9 alasiri Uwanja wa Taifa
Jumatano- Julai 10 mwaka huu Saa 9 alasiri Uwanja wa Taifa
Alhamisi- Julai 11 mwaka huu Mapumziko
Ijumaa- Julai 12 mwaka huu Saa 10 jioni Uwanja wa Taifa
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment