Kocha
wa Taifa stars Kim Paulsen akiwa na kijana wa kazi, nahodha Juma Kaseja
ambapo wawili hao watakiongoza kikosi cha Stars, huku Warundi wakiwa
mahakimu
Na Boniface Wambura, TFF
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Burundi
kuchezesha mechi ya kwanza ya mchujo ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji
wa Ligi za Ndani (CHAN) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Uganda (The
Cranes) itakayofanyika Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Waamuzi
hao ni Thierry Nkurunziza atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake
watakuwa Jean Claude Birumushahu na Pascal Ndimunzigo. Mwamuzi wa akiba
(fourth official) ni pacifique Ndabihawenimana.
Kamishna
wa mechi hiyo Gebreyesus Tesfaye kutoka Eritrea. Tesfaye pia ni
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Eritrea na mjumbe wa Kamati
ya Maandalizi ya Mashindano ya CHAN.
Wakati
huo huo, shirikisho la soka Tanzania TFF, limesema Fainali za michuano
ya Airtel Rising Stars kwa wavulana na wasichana zinazochezwa kesho
(Julai 6 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam
zitaoneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha SuperSport.
Mechi
za fainali ambazo mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Amos Makala zitachezwa kuanzia saa 7.30 mchana kwa
wasichana wakati ile ya wavulana itaanza saa 9.30 alasiri.
Nusu
fainali za mashindano hayo ambazo pia zinaonekana moja kwa moja
SuperSport zinachezwa leo (Julai 5 mwaka huu). Kwa upande wa wasichana
ni kati ya timu za Kinondoni na Kigoma wakati Ilala inaumana na Temeke.
Kwa
upande wa wavulana nusu fainali ya kwanza ni kati ya Mwanza na Ilala
ambapo baadaye itafuatiwa na nyingine kati ya Morogoro na Kinondoni.
Mechi za kutafuta mshindi wa tatu zitachezwa kesho asubuhi (Julai 6
mwaka huu).
0 comments:
Post a Comment