Keki iliyoandaliwa na Idara ya Habari- MAELEZO kwa ajili ya kuadhimisha miaka 95 ya kuzaliwa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela.
Afisa Habari Mkuu wa Idara ya Habari- MAELEZO, Anna Itenda akitoa maelezo mafupi jinsi alivyofanya kazi na Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela pamoja Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi wa idara hiyo ,Zamaradi Kawawa.
Afisa Habari Mkuu wa Idara ya Habari- MAELEZO, Anna Itenda akikata keki wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha miaka 95 ya kuzaliwa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Mzee Nelson. Keki hiyo iliandaliwa na Idara ya Habari- MAELEZO
Afisa Habari Mkuu wa Idara ya Habari- MAELEZO, Anna Itenda akimlisha keki Afisa Habari Mwandamizi wa idara hiyo , Jovina Bujulu wakati wa hafla fupi ya kuadhimisha miaka 95 ya kuzaliwa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela , huku waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakifurahia hafla hiyo iliyoandaliwa na Idara ya Habari- MAELEZO .
Picha zote - Hassan Silayo – Maelezo.
0 comments:
Post a Comment